SoC02 Katibu wa Mbunge ni mtumishi hewa

SoC02 Katibu wa Mbunge ni mtumishi hewa

Stories of Change - 2022 Competition

Erick Ezekiel

New Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Maisha yanabadilika jamii inaelimika na kupata maarifa mapya mbivu na mbichi sasa bila kikwazo tunajua kuzitofautisha, Ofisi ya Mbunge kila jimbo huwa ina mtu ambaye anafanya shughuli kwa niaba ya mbunge akiitwa Katibu wa Mbunge, Bahati mbaya upatikanaje wake haupo wazi zaidi hutegemea na namna gani amemtendea wema mbunge alieaminiwa na wapiga kura,Kiwango cha urafiki na wakati mwingine uhusiano uliopo.

Kwa hivyo nafasi ya katibu haiangalii weledi bali fadhira ambazo hugeuka majuto kwa wapiga kura.
- kuna majimbo utakuta kutokana na ukubwa wa eneo mbunge ataweka katibu zaidi ya mmoja kulingana na ukanda .
Mfano 2015-2020 jimbo la Ngara lilikuwa na makatibu wa mbunge wawili hii kwangu sio shida zaidi naangalia utendaji kazi usiozingatia weledi mwisho wanabaki kusifia aliewapa ofisi ili asiwaondoe.

- Wananchi huamini kero za jumla kama kijiji au mitaa zinazohitaji utatuzi kutoka serikalin zinafaa kupokelewa na mbunge lakin kila wanapobisha hodi hupokelewa na katibu ambae hawezi kuwa na kauli ya matumain zaidi ya kusema " nae Kumjulisha'' wenye shida hapa jibu hakuna maana kama ni kero hata sema zaidi atamwambia kuhusu pongezi na waliopita kumsalimia.

Njia bora ya kutoka hapa ni ,
-Nafasi ya katibu wa mbunge izingatie weledi katibu awe mtalam nwenye kusaidia kushauri kwenye utendaji wa Mbunge na utatuzi wa kero za wananchi.

- Kama nchi iwe na mwongozo rasmi unaowezesha upatikanaji wa katibu wa Mbunge ili uwe wazi kwa wananchi ikibidi iwe ajira sio Zawadi.

---Mwisho---
 
Upvote 0
Back
Top Bottom