Pre GE2025 Katibu wa UVCM Dar awaonya vijana wa CCM kuhusu kujigawa kimakundi wanapoelekea kwenye Uchaguzi

Pre GE2025 Katibu wa UVCM Dar awaonya vijana wa CCM kuhusu kujigawa kimakundi wanapoelekea kwenye Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Hussein Egobano, amewasihi vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiepusha na makundi ya uchaguzi na badala yake waendelee kudumisha mshikamano na umoja ndani ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Egobano ameyasema hayo tarehe 26 Februari, 2025, alipokutana na vijana wa CCM katika Ofisi za Kata ya Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayolenga kuimarisha jumuiya na kuhakikisha vijana wanazingatia misingi ya chama.

"Chama chetu ni kimoja, na ushindi wetu unategemea mshikamano wetu. Tusijihusishe na makundi yanayovuruga umoja, bali tuendelee kuwa waaminifu kwa CCM na kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama," alisema Egobano.

Aidha, aliwasisitiza vijana kuwa na subira na kutumia fursa zilizopo kwa kufuata taratibu za chama.

"UVCCM ipo kwa ajili ya kuwasemea vijana na kuwawezesha kushiriki katika uongozi. Kama una sifa, jitokeze kwa utaratibu unaostahili badala ya kujiingiza kwenye migawanyiko isiyo na tija," aliongeza.

Mwisho, Egobano amewasihi Vijana hao kujiandaa kwa ajili ya zoaezi la Uandikishaji na Uboreshaji wa Taarifa kwenye Daftari la kudumu la Mpiga kura litakaloanza tarehe 17 Machi, 2025 kwa mkoa wa Dar es salaam

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

uvccm dar.png
 
Back
Top Bottom