Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu wa Baraza la Wazee wa Jiji la Arusha, Mzee Amimu Ngalawa, ameomba serikali kuongeza kiwango cha pensheni kwa wastaafu, akisema kiasi wanacholipwa ni kidogo na hakiendani na muda waliotumikia kulinganisha na marupurupu wanayopata wabunge baada ya kuhudumu kwa miaka mitano pekee.
Akizungumza katika hafla ya uhamasishaji wa elimu ya nishati safi kwa viongozi wa baraza hilo, Mzee Ngalawa alieleza kuwa ongezeko la pensheni lililotolewa hivi karibuni bado ni dogo na halitoshelezi mahitaji ya wastaafu.
"Pensheni ni ndogo kweli kweli, hata kama mmeongeza lakini ni kiasi kidogo sana. Wazee wametumikia miaka zaidi ya thelathini au arobaini, halafu unampa shilingi laki moja. Lakini mbunge anafanya kazi kwa miaka mitano na anapata kiwango kikubwa. Hebu angalieni sisi wazee tumeteseka mno, tumefanya kazi nyingi, muwe mnatuonea huruma," alisema Mzee Ngalawa.