Katika harakati za kubandika kucha bandia na kupaka rangi kucha za akina dada

Mimi Melki

Senior Member
Joined
Mar 31, 2022
Posts
155
Reaction score
259
Habari,

Lengo la huu uzi ni kuwashirikisha kuhusu kazi ya kujiajiri ya kubandika kucha bandia na kupaka rangi za maji kucha za akina dada na wake za watu katika suala zima la urembo!

Ujuzi nilionao mpaka sasa ni kubandika kucha bandia na kupaka kucha rangi za kawaida hapa jijini Dar es salaam na biashara yangu nitaanza kwa kupita mtaa hadi mtaa, nyumba hadi nyumba, guest hadi guest na baa hadi baa!

Natarajia kuanza kuifanya nikiwa na malengo makubwa sana niliyojiwekea, hivyo ninatarajia kutengeneza pesa isiyopungua elfu kumi na tano kwa siku! Wazoefu wanambie kama inawezekana kutengeneza hiyo faida

Baada ya kuwa mzoefu na kupata pesa za kutosha, nitakusanya wateja wangu pamoja na kupanga chumba cha kawaida tu ili kuepusha gharama ya flem! Hapa nitakuwa nikifanya massage za nyayo, kuosha miguu, kupaka rangi za Gel, kusugua gaga na huduma nyinginezo muhimu

Nategemea wanawake waje waseme kwa hapa Dar nianze kuzungukia maeneo gani ambapo nitapata wateja!

Pia naombeni changamoto za biashara hii ili niwe tayari kuzikabili kutoka kwa wateja ikiwemo hata matumizi ya mafuta ya taa ili kupunguza mihemko pamoja na matumizi ya bastola ili kuepuka utatuzi!

Pia itapendeza nikipatiwa gharama ya kubandika kucha na upakaji rangi kucha ambazo mnatozwa (akina mama) ili niweke ofa kuwavutia wateja!

Muhimu:
Tumshukuru Rais!
 
Bei hutegemea na maeneo utakayokua wafanyia biashara yako
Kile la kheri
 
Nasubiria wajuzi maana wengine kushikwa miguu,kubandika kucha ni shughuli ngumu
 
Kuna member humu alinusurika kuuawa na mjeda kwa kazi kama hiyo unahotaka kuianzisha!
 
Story yako inaenda mbele hatua 10 na kurudi nyuma hatua 15. Biashara umeanza au ndio unataka kuanza?
 
Story yako inaenda mbele hatua 10 na kurudi nyuma hatua 15. Biashara umeanza au ndio unataka kuanza?
Kwa hapa Dar ndo nataka nianze rasmi wiki ijayo! Ila nimewahi fanya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…