Ungeanza kutueleza wewe mh. Mbunge mtarajiwa.
nilitolewa berenge mbaya sana usiku, na mama wa binti niliekua namfukuzia baada ya huyo maza kushtukia kwamba mimi sikua mlevi wala, mnywa pombe pale kilabuni kwao, nyumbani, bali nilikua nammendea binti yake tu,
maza alienda kushtaki hadi shule ya kata niliyokua nasoma, lakini akashindwa kunitambua kwenye parade la ukaguzi na utambuzi wa wazi pale shuleni,
naishukuru sana ile pisi kali kwa kunisitiri kwa kunikana waziwazi kwamba hakua ananijua, licha ya kwamba ni yenye ndie alieniita kilabuni kwao kwamba nizuge kama nakunywa kunywa, kuvuta muda kidogo, pakitulia wateja wakipungua nisepe nae magetoni, kumbea maza aliusoma mchezo kitambo sana...
vinginevyo ningepoteza masomo shuleni, wananchi kule jimbomi wangekosa kiongozi makini, na humu JF huenda nisingekua mtu wa watu, wa aina hii, dah....
ile pisi iko kanda ya ziwa bana inaendelea na shughuli zake tu...
