Guru Master
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 226
- 594
tunapoishi tunaishi tukijiandaa kwa ajili ya kitu kimoja tu. maandalizi yetu sote yangepaswa yawe kwa ajili ya siku ya kufa. inawezekana mara nyingi kutokana na uzuri wa maisha kwa wengine husahau kuwa kifo kipo.
Kwa nini uogope Kifo?
sioni sababu ya kuogopa kifo.. ni kama unapoanza kusoma shule ni wazi unategemea kuna siku utafanya mtihani. hivyo kuanzia siku ya kwanza unakuwa tayari ukianza kujiandaa kwa ajili ya mtihani. ndivyo ilivyo kwa maisha. maisha haya ni kama tumeazimwa tu.
binadamu tumepewa akili na maarifa angalau tuweze kufikiria namna ya kupunguza vifo visivyo na lazima ila mwishowe vifo hutokea. haijalishi uwe tajiri kiasi gani, uwe na akili kiasi gani, uwezo maskini kiasi gani utakufa.
Je kuna uwezekano ukawa na dhambi duniani ila ukifa uka bargain na Mungu?
HAKUNA.
ukishakufa umekufa. huna uwezo tena wa kwenda ku bargain na Mungu. hata dunia nzima ingefunga na kuomba, hata dunia nzima ingelia na kuomboleza lakini imeandikwa katika
Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.
siku unayokata roho tayari unakuwa umeingia hukumuni. na hukumu yako inakuja kwa matendo uliyoishi duniani. si kwa mambo mengine yeyote. ikiwa siku ya mwisho ulitubu dhambi zako ni kheri kwako Mungu wetu husamehe. sababu ni mwingi wa Neema na Rehema. lakini ikiwa ulikufa katika dhambi zako. haijalishi Maaskofu,Mapadre,Wachungaji,Wazee wa Kanisa, Waimba Kwaya Maarufu, Manabii, Mitume na Viongozi wakubwa kiasi gani watahudhuria mazishi yako na kukufanyia maombi.
kufa ni mara moja tu na mara ufapo unaingia hukumuni.
Biblia inajitosheleza. kibinadamu katika imani zetu tuliamua kuchukua mafundisho ya kipagani na kuyaingiza kwenye ukristo. ilhali biblia yenyewe inajitosheleza kwa kila jambo tulilo nalo katika maisha haya. tusi hangaike kubargain na Mungu tunapoondokewa na Mmoja ya mtu tuliye mpenda. tunajua inaumiza sana kupoteza mtu umpendaye na unatamani kwa sababu moja au nyingine kusawazisha na kusuluhisha yale ambayo ulimkosea akiwa hai au sababu ya kujisikia kuhukumiwa moyoni unaamini ukimwombea awekwe mahali pema pengine nawe atakusamehe au utasamehewa na Mungu.
hata dunia nzima ingepaza sauti kuwa huyu awekwe mahali pema. kama hakutenda yanayo mpendeza Mungu haitasaidia. kwa nini ? Mungu ni wa haki. huyu aliyefariki anaombewa na Maaskofu,Wachungaji ,Mapadre na Mwatu wengi.. je akifa maskini ambaye hafahamiani n hao wote itakuwaje? ACHENI KUSEMA R.I.P sababu haisaidii hata kumsogea nusu nchi ya sehemu aliyowekwa kutokana na matendo yake aliyotenda akiwa HAI.
na kuanzia kwenye kifo chake sisi tulio hai tunapaswa kuishi kulingana na maneno ya Mungu. kama marehemu alikuwa na dhambi mpaka anakata roho atawekwa sehemu anayostahili kulingana na maisha yake hapa duniani. hakuna sehemu ambayo roho yake itakaa kwanza kusubiri nguvu ya maombi ya walio hai kabla ya kupelekwa hukumuni.