Katika hili Wakristo tumepotoka

Katika hili Wakristo tumepotoka

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Habari wakuu!!

Mimi ni Mkristo. Tena si yule Mkristo wa kufuata miujiza au wa kufuata mkumbo. Ni mkristo ninayefuata misingi ya maandiko matakatifu kama yanavyosema bila kujali ni nini naamini au nani anaamini. maandiko matakatifu ndio msingi wa maisha ya binadamu wawapo hapa duniani. Kufuata maoni ya watu ni moja ya ukengeufu wa watu wengi hasa sisi Wakristo.

"YESU SIO MUNGU NA HAJAWAHI KUWA MUNGU, NA HATAWAHI KUWA MUNGU"

Wakristo wamejikuta wakivunja moja ya sheria za Mungu bila ya wao kujijua. Moja ya sheria za Mungu ni kutokuiabudu miungu mbinguni bila kujali inaishi wapi na inauwezo kiasi gani. Ngoja ninukuu:
Kutoka 20:
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Maandiko hayo yanatutaka tusiabudu miungu mingine. Wakristo tumejikuta tukiingia katika mtego bila kujijua. Wengi wanamhusisha Yesu na Mungu. Wengi wanamuabudu na kumtumikia iwe kwa kujua au la. Lakini ukweli ni kuwa wanavunja sheria hii kubwa ya Mungu. Sababu kubwa ya wao kumuita Yesu ni Mungu bado haipo dhahiri zaidi ya mahaba na imani iliyokosa akili na elimu ya dini. Yesu hawezi kuwa Mungu eti kwa sababu alikufa akafufuka, Alizaliwa bila mbegu ya baba, eti kisa alifufua wafua, kisa alitembea juu ya maji. Nasema hakuna kigezo kinachomfanya Yesu kuwa Mungu.

Yesu ni kiumbe kama walivyoviumbe wengine. Uwezo wake haumfanyi kuwa Mungu. Hata Musa kutenganisha bahari haikumfanya aitwe Mungu. Uwezo wa mtu, akili ya mtu na sifa zinginezo alizonazo mtu hazimfanyi kuwa Mungu. Bali zinamfanya awe mkuu kwa watu au viumbe husika.

Jukumu alilopewa Yesu ni kuitiisha Dunia kwa kurejesha utawala wa Mungu Duniani. Hata hivyo jukumu alilopewa Yesu kama kiumbe chenye heshima katika falme za kiroho ni kuiangusha mamlaka ya Shetani, kumkabili adui Mauti ambaye ndiye adui wa mwisho baada ya lucifa kuwekwa chini ya ulinzi. Na hilo ndilo jukumu la Yesu kuja kuukomboa ulimwengu kutoka katika maadui wawili yaani Shetani ambaye humtumikia Mauti. Hivyo ni kusema Mauti ndiye adui Mkuu ambaye shetani humtumikia.

Zingatia maneno niliyoyakoleza
Soma 1Wakorintho 15:
24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Ndugu zangu Wakristo tuache kuabudu Miungu bila kujijua. Yesu ni kama viumbe wengine. Tunachopaswa ni kumheshimu tuu kama viumbe wengine watakatifu. Hatupaswi kumtumikia Yesu wala kumuabudu isipokuwa Mungu pekee kama Amri za Mungu zisemavyo.

Kama kuna mwenye hoja tafadhali aje na maandiko sio maneno matupu tuu.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom