Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,138
Kwa mtazamo naona katika katiba mpya wabunge wabaki na kazi yao ya ubunge wasiwekwe kwenye nafasi yoyote inayoweza kuleta mkanganyiko nafasi hizo ni kama uwazir, ukuu wa mkoa na wilaya, wajumbe wa bodi za mashirika ya uma.
1. itasaidia kupunguza vurugu za kugombea ubunge kwa ndoto za kuja kuteuliwa kuwa waziri au naibu waziri.
2. Itasaidia kamati za bunge kufanya kazi zake ikiwa huru bila mkanganyiko kwani iwapo kamati ya bunge inakagua shirika la uma na ikatokea mwenyekiti wa bodi ya lile shirika ni mbunge unategemea nini hapo??
3. Itasaidia Bunge kuibana serikali hasa wakati wa budget kwani watakaowasilisha bajeti si wabunge wenzao kama ilivyo sasa.
4. kutoa nafasi za ajira kwa wengine kwani kitendo cha kumchagua mbunge kuwa waziri au mkuu wa mkoa ni kuziba nafasi ya wengine ambao hawana ajira.
5. Itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwani kwa upunguani tulio nao hatujaweza kutofautisha matumizi ya chama na serikali hasa pale inapotokea mbunge kwenda kwenye jimbo lake hutumia gaharama za serikali kama waziri lakini wakati huo huo anafanya kazi za ubunge wa chama chake mfano hai ngeleja.
6. Itasaidia kupunguza posho mbilimbili, anapokea ya ubunge hapo hapo atapokea posho kama waziri
7. Nafasi za manaibu waziri zisiwepo kama wizara ina waziri, katibu mkuu, mkurugenzi wa wizara sioni haja ya kuwa na naibu waziri.
Mambo mengine muhimu ni:
1.Mkurugenzi wa usalama wa taifa,
2.mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
3. Jaji mkuu,
4. mkurugenzi wa Takukuru
5. Mwanasheria mkuu wa serikali
6 Mwendesha mshtaka mkuu (DPP)
7. Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi
Pamoja na wengine niliowasaha ntakuja kuwataja mbele wasiteuliwe na Rais hawa wateuliwe na kamati maalum itakayoridhiwa na wananchi kupitia bungeni hii itasaidia wateuliwa kutenda haki bila upendeleo au shinikizo kutoka kwa rais na serikali yake nadhani yanayotokea sasa hivi wote tu mashaidi.
Pia KATIBA hii iweke adhabu kali kwa wote hasa viongozi wa uma watakaobainika kukwepa kodi, kufanya ubadhirifu wa mali za uma, kula rushwa.
Iondoe nafasi ya Makamu wa rais kwani zaidi ya kutaliii sijui majuku yake ambayo yana manufaa kwa taifa.
Yapo mengi lakini kwa leo naona inatosha tutaendelea kutoa maoni kuboresha na kupunguza yale tunayoyaona yatatutoa katika kadhia hii. Mwenyezi Mungu atuongoze tuifranikishe kwa amani