Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
MTU MMOJA TU ASIYE NA SIFA ANAPOANDIKISHWA KUPIGA KURA ANAWEZA KUVURUGA UCHAGUZI MZIMA
Utangulizi
Kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha sheria ya taifa ya uchaguzi, sura ya 343 pamoja na kifungu cha 15(1) cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mtaa, sura ya 292, ili mtu aweze kuandikishwa kuwa mpiga kura anatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi na awe raia wa Tanzania. (Tume ya uchaguzi www.nec.co.tz)
Licha ya sheria za uchaguzi nilizo zitaja hapo juu, kueleza wazi sifa za wanaotakiwa kuandikishwa kupiga kura kuwa ni watu gani. Lakini katika uhalisia utaratibu wetu uliopo hivi sasa wa uandikishaji wa wapiga kura ni tofauti sizani kama unazingatia sheria hizo, yani kwa asilimia kubwa nikama vile unazingatia tu wale watu wanaojua lugha ya kiswahili, yani mtu ukijua tu kiswahili na kuweza kutaja majina yako na unapoishi basi wewe moja kwa moja unaandikishwa kupiga kura.
Kwanini nasema utaratibu uliopo ni kama vile unazingatia tu watu wanaojua kuongea kiswahili, ni kwasababu mara nyingi watu wanaoenda kuandikishwa kupiga kura, huwa hawahakikiwi na kuthibitishwa taarifa zao kwamba je wanazosifa zote kisheria au kwamba taarifa zao wanazozitoa ni za ukweli au za uongo. Yani utaratibu uliopo mtu ukifika kwenye kituo cha kujiandikisha wewe unataja tu majina yako na baada ya hapo unachukuliwa alama za kielektroniki na kupiga picha alafu unapewa kadi ya mpiga kura kisha unaondoka zako nyumbani. Yani hata bila kuhakikiwa na kuthibitishwa taarifa zako ulizotoa, hapa kunakuwa kuna kukiukwa kwa sheria za uchaguzi kama mtu huyo atakuwa labda ametoa taarifa za uongo na hana sifa kisheria, yani hapo ni kama vile utaratibu wetu umezingatia kwenye kuongea kiswahili pekee.
Kuna ushahidi mkubwa kuwa watu wengi waliandikishwa hata katika chaguzi zilizopita bila kuhakikiwa taarifa zao, kiasi kwamba hata mtu yoyote ukimuuliza kuhusu utaratibu wa uandikishaji wa wapiga kura katika kipindi kilichopita ulivyokuwa. hapo lazima atakujibu hatukuhakikiwa wala kuthibitishwa wewe ukifika kwenye kituo cha kujiandikisha ni mwendo wa kuongea kiswahili basi mwenyewe unaonekana ni mtanzania.
Kwa hakika katika zama hizi tulizopo mtu yoyote yule anayejua lugha ya kiswahili mara nyingi huchukuliwa kama vile ni mtanzania halisi na yule asiyejua kiswahili huyo huchukuliwa kama siyo mtanzania, lakini kumbe katika uhalisia haiko hivyo, tunapaswa kuboresha utaratibu wetu uliopo wa uandikishaji kwasababu kwasasa ni kama vile unazingatia tu kiswahili na siyo sheria. Alafu siyo kwamba waandikishaji huwa wanasahau kuhakiki taarifa za watu, bali ndio utaratibu wetu wa uandikishaji ulivyo. sasa katika utaratibu huu kuna watu wanaweza kuandikishwa ambao hawana sifa.
Hebu kwanza turudi kwenye sheria. Je, sheria za uchaguzi zinawataka watu wanaondikishwa kupiga kura wawe na sifa gani, wanatakiwa wawe watanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea. Lakini vipi kuhusu utaratibu wetu wa uandikishaji uliopo, yani mtu anaenda tu kuandikishwa akiwa mikono mitupu. Je, unazani tutawezaje kumtambua mtu huyo kuwa anazo sifa zote kisheria kama tukimuandikisha bila kuhakiki taarifa zake. pengine niwazi kuwa utaratibu wetu wa uandikishaji unaigeuza sheria kuwa kama kivuli tu, lakini kumbe utaratibu wetu unazingatia vitu vingine. Hapo sasa tunakuwa tumefanya nini, tunakuwa tumeiweka sheria lakini hatujaijengea uwezo na utaratibu mzuri wa kufanya kazi yanisheria ipo kama pambo tu.
Ukweli ni kwamba sio kila mtu anayejua tu kuongea kiswahili ni mtanzania aliye na sifa za kuandikishwa kupiga kura, na sio kila mtu mnene amefikisha umri wa miaka 18. Tusijekuwa tunawaandikisha watu wasio na sifa kisheria bila kujua kwasababu kwenye utaratibu wetu hatuwahakiki taarifa zao.
Mtu yoyote yule anaweza kuzani labda kuhakiki taarifa za watu kwenye uandikishaji wa wapiga kura labda ni kitu kisichokuwa na maana yoyote au labda ni jambo la kupoteza muda, lakini bila kutambua kwamba kutokuhakiki taarifa za watu kunaweza kupenyeza watu wasio na sifa ambao wanaweza kuvuruga uchaguzi.
Kwahakika utaratibu tulionao unaweza kupenyeza asilimia kubwa ya watu wasio na sifa, kiasi kwamba mtu yoyote yule anaweza hata kutoa taarifa za uongo au anaweza kukusanya kundi la watu wasiokuwa watanzania na kuwaandikisha kwa urahisi kabisa kupiga kura, yani ilimradi tu unafahamu lugha ya kiswahili.
Mapendekezo
Napendekeza kwenye tukio la muhimu sana kwetu ambalo pengine labda tukifanya makosa linaweza kugharimu mali zetu au hata maisha yetu, tukio la kuchagua wanaoenda kuwa wasimamizi wa taifa letu la Tanzania yani kwenye uchaguzi, napendekeza tuwe na utaratibu wa kuhakiki taarifa za wale tunao waandikisha, tusijekuwa tuna waandikisha kundi la watu wasio na sifa kisheria bila kujua, hali inayoweza kuvuruga uchaguzi na kupelekea hata uwepo wa viongozi wasiobora ambao watanzania hawakuwachagua.
Nashauri watu wote watakaoenda kuandikishwa kupiga kura wasiende tu mikono mitupu, bali waende na vitambulisho mbali mbali vyenye taarifa zao ili mwandikishaji aweze kuhakiki taarifa zao kabla ya kuwaandikisha. Vitambulisho hivyo vitakavyo tumika vinaweza kuwa mfano vitambulisho vya taifa au vitambulisho vyengine vyovyote vinavyokubalika vyenye taarifa zao. Kusudi ni kuhakikisha uchaguzi wetu unabaki kuwa salama wa haki na wa wazi.
Alafu pia ningependa kuona hata wale waandikishaji wa wapiga kura wawe ni wakazi wa meoneo hayo hayo wanapo andikishia wapiga kura. Naamini kwamba itakuwa rahisi kuthibitisha taarifa za wale wanaoandikishwa kupiga kura, kama waandikishaji watakuwa wanawafahamu wanao waandikisha, yani kwa asilimia kubwa itakuwa siyo rahisi mtu kutoa taarifa za uongo. Hatua hii ni nzuri na nibora zaidi kama ikitumika kuliko ile ya kuchukua waandikishaji kutoka maeneo mengine kuja kuandikisha kwenye maeneo ya watu wasio wafahamu, kwani kuna weza kupenyeza watu wengi wasio na sifa kuandikishwa au kuwapa mwanya baadhi ya watu kutoa taarifa za uongo.
Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo itakuwa na viongozi bora na wenye sifa za kiungozi walio chaguliwa kihalali na wananchi wa Tanzania kwenye uchaguzi. wengi wetu tunaamini kwamba endapo nchi itakuwa na viongozi wabaya na ambao hawajachaguliwa na wananchi kunaweza kupelekea tuwe na Tanzania tusiyoitaka.
Niwakati sasa wa madiliko kwa pamoja tujenge Tanzania bora, lakini ili kufanikisha hili tunahitaji kupata viongozi bora pia, ambapo viongozi hawa tutawapata kutoka kwenye chaguzi zetu mbalimbali, sasa basi ni vyema kuziboresha taratibu zetu hizo ili tuweze kuwapata viongozi bora watakao tuongoza kuipata Tanzania bora tuitakayo. Hivyo tunapaswa kufanya madiliko kwani ili kuijenga Tanzania bora tuitakayo ni lazima tuwe na viongozi bora tuwatakao kwanza.
Upvote
2