KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,794
- 9,075
Biden ameondoa marufuku kwa Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi
Joe Biden ameiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu ya Marekani.
Rais Biden ameidhinisha Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zinazotolewa na Marekani ndani ya Urusi kwa mashambulizi machache, maafisa wa Marekani wamesema.
Ukraine inapanga kufanya mashambulizi yake ya kwanza ya masafa marefu katika siku zijazo, duru zilisema, bila kufichua maelezo kutokana na wasiwasi wa kiusalama.
Hatua hiyo ya Marekani inajiri baada ya miezi kadhaa ya ombi la Volodymyr Zelenskyy kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha za Marekani kushambulia maeneo ya kijeshi ya Urusi mbali na mpaka wake.
Mabadiliko hayo yanafuatia Urusi kupeleka wanajeshi wa nchi kavu wa Korea Kaskazini ili kuongeza vikosi vyake, jambo ambalo limezua taharuki mjini Washington na Kyiv.
Mashambulio ya kwanza ya kina huenda yakatekelezwa kwa kutumia roketi za ATACMS, ambazo zina masafa ya hadi maili 190, kulingana na vyanzo.
Kwa Mtazamo wangu nikwamba sasa hii vita inakuja kuwa vita ya ukanda ambayo italeta maafa makubwa sana labda na sema labda kwa rais mpya atakayeingia apige marufuku kuendelea kutumia Siraha za masafa marefu vinginevyo mambo yatakuwa magu sana!