Mjuzi wa mambo
Member
- Jan 22, 2014
- 12
- 3
Katika kueleka Mwaka mmoja wa Magufuri, CCM bado yashindwa kuvilipa vyombo vya habari
Wakati Rais,John Pombe Magufuri akikaribia kutimiza mwaka mmoja tangu achaguliwe kuiongoza Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), bado kimekaa kimya juu ya madai ya vyombo vya habari vilivyotoa matangaza ya kampeni ya chama hicho.
Zimekuwa zikifanyika juhudu za makusudi kwa wamiliki wa vyombo vya habari kufuatilia malipo hayo, lakini hali imekuwa tofauti na pindi walipokuwa wakivipigia magoti vyombo hivyo kufanya cavarege nzuri za kampeni za CCM.
Ijapokuwa CCM ndicho chama kilichoonekana kuwa pesa nyingi kuliko vyama vingine,hali imekuwa tofauti pamoja na uwezo mdogo wa vyama vya upinzani, lakini viliweza kuvilipa vyombo vya habari mara baada ya uchaguzi huo kumalizika.
Katika shukrani zake kwenye hutuba zake mbalimbali, Magufuri amekuwa akivishukuru kwa kazi kubwa ambayo wameifanya katika kufanikisha kampeni hiyo lakini kwenye mustakabri mzima wa kuhabarisha umma.
Hali imekuwa tofauti na anayosema, kwani matangazo mengi yaliyotolewa yalikuwa ni kampeni ya rais na si wabunge wala siyo madiwani na ili kuthibitisha kauli yako Mheshimiwa Magufuri vilipe vyombo vya habari.
Vyombo vya habari vimekuwa vikipiga hadi kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM yalipo Lumumba katika kuulizia malipa ya wahabari hao.
Simu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrham Kinana, Msaidizi wake Luhavi na Mweka hazina wa chama hicho,Zakia Megji zimekuwa hazipokelewi na hata wakipokea majibu yao yamekuwa siyo ya kuridhisha, jambo ambalo limekuwa na wasiwasi mkubwa wa kulipwa kwa malipo hayo.
Kabla ya Mkutano Mkuu wa CCM wa kumchangua mwenyekiti mpya wa chama hicho, CCM wamekuwa wakipiwapigia simu vyombo vya habari kwa madai ya kuhakiki matangazo hayo na kuyalipa kabla ya mkutano huo, lakini badala yake haikuwa hivyo.
Lakini lengo kubwa lilikuwa ni kuwadhihaki waandishi na kuwahada ili waweze kufanya cavarage nzuri ya mkutano wao wa Dodoma ambao waandishi walikuwa wakihamasishana wiki moja kabla kususia mkutano huo ambao Kikwete alikuwa akichia madaraka.
Hata hivyo wasanii wa muziki ambao walishiriki katika kampeni hizo, wale waliolete vifaa mbalimbali vya kampeni wenyewe ndio waliopewa kipaumbele kulipwa kutokana na umuhimu wao kwa CCM, tofauti na waandishi ambao wanaonekana hawana thamani mbele ya chama hicho kilichoshika hatamu ya nchi.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya ofisi ndogo ya CCM zinadai kuwa hatua hiyo ya kucheleweshwa kwa malipo yao inatokana na kutokuwa na uhakika wa kiasi hicho cha fedha wanachodaiwa, kiasi cha kuagiza timu maalum ya uhakiki kutoka makao makuu Dodoma kufany kazi hiyo.
Pamoja na waandishi kuonesha ushirikiano mkubwa wa uhakiki katika timu hiyo, lakini bado malipo hayo yamekuwa kama ya sinema ambayo haina mwisho.
“Tumefanya ukaguzi wetu na kujiridhisha baadhi ya madeni yanapaswa kulipwa, hivyo naomba mvute subira na malipo yenu yaandaliwa na mtalipwa hivi karibuni, alisema Mama mmoja aliyekuwa katika timu ya ukaguzi.
Haya hivyo waandishi wanashindwa kujuwa hadi lini malipo yao yatakuwa tayari , kwani isije kuwa subiri ya fisi anayesubiri mkono wa binadamu kuanguka, maana haitajwi siku wala mwezi wa kufanya malipo hayo ambayo vyombo vya habari vinategemea zaidi pesa hizo za matangazo kuendeshea kampuni zao.
Mmoja wa wamili wa vyombo vya habari kuomba Editors Forum kuandika barua kwenda CCM katika kutoa angalizo ya kupata malipo yao, la sivyo basi mgomo wa kususia habari za CCM ziendelee hadi hapo zitakapolipwa fedha zao.
Serikali ilishasitisha matangazo kwenye vyombo binafsi vya habari, hali iliyofanya vyombo vingi vya habari kjutegemea zaidi mauzo, tofauti na mwanzoni ambao matangazo nayo yaliweza kusaidia uendeshaji wa hivyo vyombo.
Hivyo kulipwa kwa fedha hizo sasa hivi kupo mikoni mwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, John Pombe Magufuri ambao ndio tegemeo lao kwa sasa,.
Uzuri ni kwamba sektarieti nzima ya chama hicho wamerudi wote, hivyo tathmini ya kuthamini madeni wote wanaijuwa,ugumu na wasiwasi ulikuwepo iwapo kama ingekuja sektarieti nyingine mpya.
Sasa wakati umefika kwa CCM kuthamini mchango wa vyombo vya habari kama vyombo hivyo vilivyotoa mchango mkubwa kuhakikisha vinashika dola.