UsalitiCOdili
New Member
- Nov 23, 2017
- 3
- 0
UTUMWA WENYE FAIDA
Jua linapochomoza, nainua macho yangu na kuitazama mbingu jinsi ilivyopendeza, hakika ni uumbaji wa kustajabisha! Nina kila sababu ya kusema ‘Asante MUNGU kwa siku nyingine’. Najivunia kuwa Mwafrika! Kuwa Mtanzania!
Kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi, mataifa mbalimbali yanatetemeshwa na majanga mbalimbali! Matetemeko ya ardhi, mafuriko, joto kali na vimbunga vya ajabu, lakini kwa sehemu kubwa Afrika imeendelea kuwa salama! Tuna kila sababu ya kumshukuru MUNGU!
Mara nyingi nimekuwa nikifurahia sana kuitumia karama hii ya kuandika ili kuzungumza na ndugu zangu ambao kwa namna moja au nyingine siwezi kukutana nao tukazungumza ana kwa ana. Naamini kupitia maandiko haya, naweza kuwafikia wengi zaidi. Naamini kila atakayefikiwa atakuwa na jambo la kujifunza; linaweza kuwa jipya au si jipya ila likakomaza tu kiwango chake cha kuelewa!
Karne ya kumi na tisa kuelekeea karne ya ishirini, ni kipindi ambacho kimebeba historia ya jasho, machozi na damu kwa wanadamu wengi hasa waishio ndani ya bara la Afrika. Kilikuwa kipindi cha utumwa wa wazi, utumwa wa mateso yasiyomithilika kwa wana wa Afrika!
Imani yangu inaniambia, dunia haiwezi kuwa salama na ya kupendeza kama hakuna mawazo yanayokinzana! Na Imani hiyo ndiyo itakayonisukuma katika kuandika makala haya!
Kila ninapoisoma historia ya bara la Afrika hasa nikiitazama Afrika Mashariki (EAC) zaidi sana Tanzania, ni dhahiri shayiri kuwa machozi yananitoka na kunifanya nijisikie vibaya kwa hali zilizowapata wazee wetu wa kipindi hicho!
Katika taswira yangu ya ndani, namuona Mkwawa akikabiliana na mkono wa chuma wa Mjerumani! Nawaona watemi mbalimbali wa Afrika wakipambana na mateso, suluba na ukilitimba wa kila namna kutoka kwa mtu mweupe! Kwa kiwango kikubwa inasikitisha sana.
Pamoja na hayo yote, najisikia faraja kubwa na kuthubutu kusema kuwa, japo ulikuwa ni utumwa mbaya ila ulikuwa ni
‘UTUMWA WENYE FAIDA’!
Kwa ujumla, historia , ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbali mbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.
Ni ukweli usiopingika kuwa, hata kabla ya kuingia kwa wakoloni, Afrika ilikuwa na ustaarabu wake yenyewe na ilijitawla kwa kuandama kanuni na taratibu maalumu zilizosimamiwa na asili!
Siku zote mazingira salama lazima yaongozwe na asili! Kama hakuna asili basi hakuna usalama! Asili hushinda yote, asili hupendeza pote na asili hutambua yote!
Nyakati zote za Afrika chini ya ukoloni, zitaendelea kuwa nyakati mbovu kabisa za mateso kuwahi kumpata Mwafrika, Lakini pia, zitaendelea kuwa nyakati njema kwa wapenda mabadiliko wote duniani!
Katika kujadili historia ya ustaarabu wa Mwafrika, Misri inasimama kama mwalimu bora kabisa!
Misri ya Kale ni ustaarabu uliokuwepo Afrika kaskazini, sambamba na mto Naili, kuanzia kwenye delta au mdomo wa Naili, toka kaskazini mwa Misri kwenda kusini hadi Jebel Barkal, kwenye maporomoko ya nne, wakati wa kupanuka kwake (Karne ya 15 KK). Ustaarabu huo ulidumu kwa karibu milenia tatu, toka takribani mwaka 3000 KK hadi mwaka 30 KK nchi ilipovamiwa na Waroma na kuwa sehemu ya Dola la Roma.
Uti wa mgongo wa Misri ya Kale ulikuwa mto Naili. Sehemu kubwa ya nchi hiyo ni jangwa lakini umwagiliaji wa mashamba kwa njia ya maji ya mto ulileta mazao mazuri yaliyolisha watu wengi. Nahapo ndipo unapoweza kuona picha halisi ya Afrika hata kabla ya uvamizi wa wageni.
Ujio wa wageni katika bara la Afrika siyo na haupaswi kutajwa kama kitovu cha ustaraabu wa Mwafrika. Historia inakana hilo japo wale wanaojiona bora (Superior) wanajitahidi kuiaminisha dunia kuwa Afrika ni bara la giza na wao ndiyo walileta ustaarabu!
Kwa sisi tulio wengi tumeaminishwa kupitia mafundisho ya vitabu vya watu weupe, yaani wazungu na waarabu, kuwa ma-Pharaoh wa Misri walikuwa ni watu wenye asili kama ya kwao ,yaani weupe, na kwamba ma-pyramid yalijengwa na jamii iliyokuwa na maendeleo ya hali ya juu sana na haiwezekani hata kidogo watu hao wakawa ni watu weusi, yaani waafrika
Aibu imewakuta watu weupe na wataalamu wanaojiita Egyptologists walioamini kuwa mtu mweusi -negro hana uwezo wa hata kuwa na maarifa yanayo fanana na Misri ya ma-pyramid, kifupi wameumbuka na wameumbuliwa na technolojia yao wenyewe, yaani DNA Sequencing.
DNA ya Pharaoh Ramses III imethibitisha farao huyu alikuwa mweusi pii!, tena asili yake ni hapa Afrika Mashariki. DNA yake imepewa jina,inaitwa E-V38. Kinasaba hiki cha E-V38 kinapatikana kwenye damu za wanaume wa Afrika, hasa afrika mashariki na si kwingineko. Huu ni uthibitisho mwingine kuwa ‘UTUMWA WETU UMEKUWA WENYE FAIDA’.
Ipo siri kubwa sana inayoambata na utumwa! Kwa kawaida kabisa, mtumwa anachukuliwa ni mtu dhaifu asiyeweza kufanya kitu chochote kilicho bora! Na wakati huo, aliyesababisha uwepo utumwa, daima anafanya kila linalowezekana azidi kufifisha historia ya mtumwa wake ili aendelee kumtawala zaidi! Na huo ndiyo mchezo unaoendelea katika dunia ya leo! Ukoloni mamboleo! Ishukuriwe asili, hairuhusu dhuluma iendelee!
Kadri harakati za kuimarisha ukoloni zilivyozidi kupamba moto, ustaarabu wa Mwafrika uliendelea kuenea na utaarabu wa weupe nao uliendelea! Mchanganyiko huu wa kitabia, huku tabia ya weupe ikionekana ndiyo bora zaidi (Kutokana na mikakati ya weupe), ulifanya Mwafrika apate mbinu zaidi ya kuwatambua adui zake wakubwa!
Vita haiwezi kuisha kama hautamtambua adui yako! Hauwezi kushinda vita bila kujua kwa nini uko vitani na kwa kipindi gani utatakiwa kuwa vitani! Ilikuwa ni muhimu na lazima Mwafrika atambue kuwa, adui yake mkubwa siyo mweupe bali wepesi wake wa kupokea kile kilichoitwa ustaarabu wa weupe na kuanza kuukana ustaarabu wake mwenyewe!
Hata katika dunia ya leo hasa Afrika, wananchi wameendelea kuishi katika mateso makubwa kutokana na tabia yao ya ‘ndiyo mzee’bila kuhoji. Kama upo utumwa mbaya basi ni utumwa wa kuishi kwa kukubali kila kitu bila kuhoji au kujaribu kuhoji!
Ni ukweli usiopingika kuwa Afrika imepitia katika kipindi kibaya sana cha kutawaliwa (direct)! Ni ukweli kwamba kwa macho ya kawaida, yalikuwa ni mateso makubwa sana yasiyoelezeka! Ni kweli kwamba ilikuwa ni aibu kubwa! Lakini pia, ni ukweli mwingine mzuri kutambua, ule ulikuwa ‘UTUMWA WENYE FAIDA’!
VUTA PICHA HII
Mtoto ana miaka sita ya kuzaliwa! Mtaani kuna mambo mengi anayafurahia, kama vile kucheza na wenzake, kula na kufanya mambo yake anayoyafurahia kama mtoto! Ghafla siku moja anaamka asubuhi, anakuta kuna nguo maalumu, anaambiwa ajiandae kwenda shule! Shule!
Anaanza kupangiwa ratiba ya kuamka! Ratiba ya kula! Nguo za kuvaa kwa wakati maalumu! Ni utumwa ila ‘UTUMWA WENYE FAIDA’! Utumwa unaomfanya mtoto aache vitu anavyovipenda ili akafanye vitu wanavyopenda walioamua aende shule! Huu ni mfano unaoonesha kuwa hakuna mwanadamu anayeishi maisha huru kwa asilimia mia moja! Kila mwanadamu ana utumwa wake! Kwa wakati wake na kwa hatma yake mwenyewe! Ni hatma njema au mbaya! Inategemeana na mapokeo pia uwezo wake wa kutambua kwa nini yuko katika huo utumwa! Nakuhakikishia, motto huyo, pamoja na fimbo, adhabu na madhila mengine atakayokutana nayo, hatma yake haiku katika kuyafikiria hayo ila katika kufikiria maisha baada ya hayo (maisha ya shule).
Nchi nyingi za Afrika ziliathiriwa na zimeendelea kuathiriwa na utumwa chini ya mtu mweupe, kwa sababu hazijatambua asili yake na hazijawahi kuwaza maisha nje ya utumwa! Bajeti nyingi za mataifa ya Afrika zinaonesha utumwa kuliko ule utumwa uliowahi kuwepo!
Kama upo utumwa mbaya basi ni utumwa unaoendelea kuwepo hata baada ya mtumwa kutambua kuwa hastahili kuendelea kuwa mtumwa tena! Na hapo ndipo Afrika imebaki kusimama!
Afrika imeendelea kupitia wakati mgumu! Uhuru wa bendera ndiyo umekuwa kiini macho kwa watawala wengi wa Afrika! Wanaendelea kuwa watumwa chini ya weupe. Hadi sasa ukiangalia, watawala wa Afrika wanasimama kama wanyampala wanaowaswaga wafungwa wenzao (wananchi) kutimiza matakwa ya mkuu wa gereza (weupe). Na huu ndiyo ‘UTUMWA USIO NA FAIDA’! Kuwa mtumwa wakati unatambua haustahili kuwa mtumwa!
Katika utumwa wa kale, Mwafrika aliaminishwa kuwa mweupe ndiye binadamu bora anayestahili kutawala kila kitu! Nakuhakikishia huo ulikuwa ‘UTUMWA WENYE FAIDA’kwa sababu, siku Mwafrika alipogundua anadanganywa, ndiyo siku alipotambua thamani yake na kuamua kupambana kutafuta uhuru wake!
Ni kweli alilima mashamba ya weupe usiku na mchana! Lakini alipata mbegu ya mahindi akaongezea kwenye mazao yake ya mtama! Ni kweli alishurutishwa kupigana vita za bwana wake! Akapata ujuzi wa kutumia silaha na akajua mbinu mpya za vita! Ikumbukwe wakati huo, Mwafrika hakuwa na haki ya kujieleza, hivyo mbinu zake za vita hazikujulikana sana kwa wageni! Hii ni tofauti na saasa ambapo, viongozi wetu ndiyo watumwa wakuu (Manyampala), wanatoa siri za vyumbani ili wajihakikishie ushindi dhidi ya ndugu zao
Waafrika ambao ni washindani wao kisiasa!
Utumwa huu wa sasa ndiyo utumwa mbaya zaidi! Tayari mweupe anajua, Mwafrika naye anajua! Juhudi za mweupe ni kuhakikisha anatumia zile chembechembe za kale, alizopanda kwa Mwafrika kuwa mweupe ndiye kiumbe bora zaidi (superior) duniani! Baadhi yetu tunaamini na tunaendelea kuamini hivyo! Mweupe anatumia kila mbinu kuhakikisha mambo yake yanakuwa ya siri sana kwa Mwafrika!
Hata sasa ushahidi upo wazi! Wadada na wakaka wa Kiafrika wanaojiona bora zaidi, wamelazimika kujichubua ili waonekane weupe! ‘UTUMWA USIYO NA FAIDA’! Ishukuriwe asili, hairuhusu wawe weupe ila inawafanya wawe ‘vinyago’ mbele ya weupe!
Afrika iliyowahi kuwa uwanja wa watu wake kuburuzwa, Afrika iliyodharaulika, leo imesimamisha Rais wa Taifa lenye nguvu duniani! Ina madaktari bingwa wa kuheshimika katika mataifa yaliyoendelea! Na ukiangalia utagundua kuwa, weni ni mazao ya watumwa wa kale! Kwa namna gani utanishwaishi kuwa ule hakuwa ‘UTUMWA WENYE FAIDA?’
Utumwa unaokufanya uishi dunia mpya! Utawale katika ardhi yao! Utumwa unaokufanya upate ujuzi wao! Utumwa unaokufanya uwaambukize mitazamo yako! Utumwa unaokufanya uwe na kizazi bora katikati yao! ‘UTUMWA WENYE FAIDA’
Leo wanaimba Hip hop! Wanaimba Reggae! Wanacheza sinema ambazo ni asili ya mfumo wa simulizi za zamani za wazee wetu! Hakika ni ‘UTUMWA WENYE FAIDA’ Hatupaswi kujutia fursa hiyo! Ni kweli ilikuja kwa mateso lakini imekuwa na faida kwetu!
Najua wapo watakaopinga na kusema, Afrika ilinyonywa! Haikupaswa kuwa hivi ilivyo! Weupe wameharibu rasilimali zetu! Swali la kujiuliza, hata baada ya weupe kuondoka, mbona bado tunatumikishana sisi kwa sisi? Kuna utumwa mbaya kuzidi huu? Ndugu kuuwana kwa uroho wa madaraka! Utumwa upi ni mbaya, kutumia lugha ya wageni kwa lazima au kuikana lugha yko kwa hiyari?
Utumwa mbaya ni huu, serikali kupambana na watoa huduma za tiba mbadala Afrika wakati Ulaya, Amerika na Asia wanaheshimu tiba za mimea kuliko tiba za kisasa! Utumwa mbaya ni huu, Tanzania kuficha historia yake halisi ya mapinduzi yaliyoshindikana (Mwaka 1964, wakati huo Tanganyika)! Huo ndiyo ‘UTUMWA USIO NA FAIDA’
Utumwa mbaya ni huu, kumkataza ndugu yako kutoa maoni na kumruhusu mgeni siyo tu kutoa maoni bali kukupa maagizo magumu na ukayafuata bila kuhoji! Utumwa mbaya zaidi ni huu, kukataza wabunifu wote kufanya shughuli za ubunifu wa vyombo vya moto huku ukihimiza taifa la sayansi na teknolojia kwa maendelo ya viwanda!
Kama kuna kitu Afrika inatakiwa kukifanya, siyo kufanya jitihada za kufuta kumbukumbu za utumwa, bali kuziendeleza alama zote za utumwa wa kale ili vizazi vijavyo vijue kuwa, wazee wao waliwahi kutawaliwa kwa mkono wa chuma na wageni, na watumie alama hizo kutoa hukumu, kati ya utawala wa suluba kutoka kwa wageni dhidi ya utawala wa kinafiki kutoka kwa ndugu wa damu!
Kila la heri katika kila jambo. Katika yote huu ndiyo utabaki kuwa msimamo wangu, hakuna mtu atakayenishawishi kuamini kuwa utumwa wa kale ni mbaya kuliko utumwa sasa wakati pamoja na suluba zote za weupe, elimu ya wakoloni kupitia mkono wa mkoloni ilitupatia Mwalimu Nyerere, elimu ya mkoloni chini ya mikono yetu wenyewe inatupatia ‘Vilaza’!