Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Katika mpango wa kidunia unalenga kufikia 2030 Mwanamke asibakie nyuma katika maendeleo endelevu ya kidunia, juhudi mbalimbli ufanywa na taasisi za kidunia, vyombo mbalimbali katika Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika yasisiyo ya Kiserikali, wanaharakati, wanasiasa pamoja na wadau wengine wakiwa na dhumuni la kufanya mwanamke kusimama kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.
Eneo la haki za kiuchumi, kijamii pamoja na kiutamaduni limekuwa mstali wa mbele kupiganiwa na wadau hao kuhakikishi wanakuwa kwenye mzani rafiki ambao hautengenezi wiano unaodaiwa kuwa kandamizi baina yao na wanaume.
Tanzania imekuwa miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa sehemu ya utekelezaji mkakati huo unaolenga kuwezesha mwanamke kukombolewa katika minyororo inayofunga haki zake ambazo udhaniwa kuwa anazistaili.
Katika jitihada hizo sheria mbalimbali zimekuwa zikitungwa na nyingine kufanyiwa maboresho katika mlengo unalenga kulinda na kusimamia kinagaubaga haki wanawake, pia miongozo mbalimbali pamoja na kanuni zimekuwa zikitungwa ikiwa lengo ni lilelile la kusimamia kidete haki za wanawake.
Aidha licha ya uwepo wa sheria na miongozo hiyo Viongozi wa Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassani wamekuwa mstali wa mbele katika kutumia majukwaa kutoa maelekezo juu ya usimamizi dhabiti wa haki za Wanawake na kelekeza wanaonda kinyume hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Pia wanaharati, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) hususani mashirika amabayo yanatekeleza majukumu ya kulinda kutetea haki za wanawake nao wamekuwa mstari wa mbele kupaza sauti zao kutetea wanawake, wanasiasa nao hawapo nyuma katika hilo, ni mara nyingi baadhi ya wabunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakisikika wakipaza sauti zao juu ya haki za wanawake.
Msukumo huu wa kuifanya Dunia kuwa sehemu rafiki zaidi kwa mwanamke kuishi unagusa pia tamaduni ambazo zinaonekana kumkandamiza mwanamke na kumkosesha haki zake, pia mabadiliko hayo yamekuwa yakifanya wanawake kushiriki kwa usawa kwenye maswala ya kijamii hususani maswala ya uongozi katika viti vya kisiasa.
Binafsi naweza kuungana na mtazamo wa wadau wengi kuwa mwanamke anastaili kupata haki, lakini tutafakari utaratibu na mifumo inayojengwa kuwezesha upatikanaji wa haki hizo inaweka kwenye wakati gani haki za wanaume? na je, zile desturi rafiki zipo katika nafasi gani?
NINI KINAWEZA KUTOKEA UMAKINI UKIKOSEKANA?
Jamii inaweza kufanikiwa kumeza kampeni mbalimbali zinazolenga kulinda haki za mwanamke lakini haki za mwanaume zikawa katika mazingira ya kuvunjwa, mfano vipo visa na mikasa ya wanaume kupigwa na kufanyiwa matendo ya ukatili lakini imekuwa ngumu kusikika kwenye vyombo vya habari au visa hivyo kutoka nje ya familia husika.
Wapo wanaume ambao wamekuwa wahanga kutokana na kuamini dunia hipo ‘bize’ na mwanamke hivyo wao hawawezi kuripoti matukio yao kwenye vyombo husika wakihofia kuchekwa au kutopewa kipaombele katika kutafuta ufumbuzi.
Kupolomoka kwa Maadili Chanya. Zipo baadhi ya desturi na mila ambazo zimekuwa zikimzunguka mwanamke lakini zimekuwa chachu ya kulinda heshima za wanawake hususani katika Bara la Afrika, mfano suala la mavazi, hii ni miongoni mwa desturi ambayo imekuwa ikionekana kilinda thamani ya mwanamke wa kiafrika ikiwemo Tanzania.
Wanawake wanaweza kupata haki ya kuvaa mavazi ya aina yoyote hata kinyume na ilivyozoeleka kwa kudhania kuwa ni haki muhimu ambayo wanastaili lakini madhara yake yanaweza kuwa makubwa hasa kupelekea kuporomoka kwa thamani ya mwanamke ambayo imekuwa tunu kwa kipindi kirefu, hatuna budi kulitafakari kwa kina jambo hilo.
Siku hizi imekuwa sio jambo la kushangaza kusikia kijana wa miaka 18 anatoka kimapenzi na Mwanamke wa miaka 40, wengine wanaweza kuamini kuwa usemi usemao ‘’Mapenzi kipofu, Ukipenda Usikii Wala Kuona”, lakini tukitafakari kwa upana kilichopo nyuma ya pazia ni pamoja na kuporomoka kwa thamani ya mwanamke inayochangiwa na mavazi pamoja na anavyishi na jamii.
Kuongezeka kwaMatukio,Visa na Mikasa ya Uvunjifu wa Haki za BInadamu.* Katika kipindi cha hivi karibuni kwenye familia nyingi kumekuwepo matukio mengi ya kusitaajabisha, miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na vipigo baina ya wanandoa au wapenzi, unyanyasaji wa kisaikolojia ambao ikichunguzwa kwa kina kuna asilimia kubwa ikabainika chanzo cha matukio hayo ni mwanaume kuhofia nafasi yake kutawaliwa na Mke wake au mpenzi wake hivyo akitaka kujiami kulinda nafasi yake visa na mikasa ikiwemo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapo ndiyo linakuwa chimbuko.
Kuongezeka kwa Watoto ‘Wasio na Baba’ Au Wasio na Malezi ya Wazazi Wote , kutokana na ndoa nyingi siku hizi kukumbwa na matukio na mikasa kinaweza kuwa chanzo cha kuwafanya vijana wengi wa kiume na kike wasitamani kuishi maisha ya kwenye ndoa, watoto wanaozaliwa wamekuwa wakishudia matukio yanayofanya na wazazi wao mbele yao, watoto hao lazima wakumbane na kizungumkuti mbeleni kuamua kuoa au kutokuolewa, siku hizi baadhi ya wanawake wamekuwa wakipinga vikali suala la kuolewa wakiamini ndoa ni uwanja wa vita, lakini pia baadhi ya vijana wa kiume wamekuwa wakiamini ni bora zaidi kuzaa na mwanamke akiwa nje ya ndoa (kutoishi wote kifamilia) kuliko kukaa wote, baadhi ya sabubu ambayo imekuwa ikitajwa ni pamoja na mmomoyoko wa kimaadili kwa baadhi ya wanawake katika ndoa, hali hii inaweza kupelekea baadhi ya watoto kukosa malezi na ya Baba zao au kutelekezwa
NINI KIFANYIKE KUEPUKA HALI INAYOWEZA KUJITOKEZA
Kampeini za Kumkomboa Mwanamke Ziende Sambamba na Zoezi Uelimishwaji wa Wanaume.
Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya jitiada za kuendesha kampeni mbalimbli zinazolenga kumuwezesha Mwanamke kupata haki stahiki, hakuna budi hata kuwekeza nguvu nyingine katika kuwaelimisha wanaume likiwemo kundi la vijana ili kutambua dhumuni au dhamira halisi ya kumkomboa mwanamke.
Kampeini hizi zinapojikita upande mmoja bila kutoa mwanya kwa Mwanaume kuwa kwenye nafasi ya kutengeneza dhana yenye tafsiri tofauti juu ya mwanamke aliyekombolewa hususani kujua haki zake, mfano wanaume kuna baadhi ya visa ambavyo uwatokea wanawake endapo wanapohoji juu ya maamuzi ambayo ufanywa na waume zao katika familia, wapo wanaume wanaona mwanamke kuhoji juu ya jambo fulani ambalo limefanywa na mwanaume ni kukosa maadili jambo ambalo uenda sivyo.
Elimu ikitolewa kwa wanaume wa aina hiyo itawasaidia kutambua dhamira ya ukombozi wa mwanamke, wanaume wanaoamini Mwanamke ni mtu wa kukaa nyumbani na kumbana asijiendeleze kiuchumi watabadilika na kuishi kwenye dhana halisi inayolengwa juu ya ukombozi huo na inawezekana wanaume wakawa mabalozi wema katika kulinda na haki za wanawake.
Kusisitizwa kwa Mifumo ya Sheria Ambayo ni Rafiki kwa Pande Zote.
Mifumo ya kisheria na kisera inayoedelea kutungwa isilenge kulalia zaidi kwa Wanawake badala yake yawekwe Mazingira ambayo ni rafiki kwa jinsia zote licha ya kipaombele kuwa ni kumkomboa Mwanamke lakini kusiwepo na tabaka kubwa baina ya upande mmoja na mwingine hali ambayo inaweza kupelekea changamoto mbeleni.
Jamii Hususani Wanawake Watambue Kuwa Mkakati wa Haki Sawa kwa Wote Sio Silaha ya Kudidimiza Haki za Wanaume.
Wapo wanawake ambao wanaweza kudhania kuwa mkakati unaoedelea duniani hasa kwenye mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania ni silaha inayowapa kinga ya kuvunja haki za wanaume. Katika hilo kuna umuhimu Serikali pamoja na wadau wanaoendesha kampeini za kuwakomboa wanawake ili kupata haki staiki kuwaelimisha zaidi na kuweka msisitizo katika umuhimu wa kutumia nafasi hiyo kujikomboa katika mazingira ambayo hayapelekei kuvunja haki za wanaume.
Kwa mfano kwenye jamii zetu wapo baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakibeba tafsiri ambayo ni potofu hasa baada ya kudhani kuwa wameelimika kuhusu masuala ya haki zao na hiyo inakuwa chanzo cha kutumia nafasi vibaya kuvunja haki za wanaume hali amabayo sio rafiki kwenye jamii na wakati mwingine imekuwa ikiibua migogoro.
Ni busara na hekima kwa wanawake ambao wameelimika kuhusu haki zao kutumia upeo wao kuwa mabalozi wema kwa wanawake wengine hata ikibidi kuwaelimisha wanaume mbalimbali kuhusu dhamira ya kumkomboa mwanamke kuliko kutumia upeo huo kuibua sintofahamu zisizoleta tija kwa jamii.
Muhimu, mwanamke anastaili kupata haki muhimu katika harakati za kuleta maendeleo kwa taifa lakini ni muhimu kuendelea kuzilinda haki za upande mwingine zisivunjwe, kama mamlaka, wadau pamoja na jamii zikibweteka bila kuliona hilo kwa jicho la tatu uenda siku moja, dunia ikiwemo taifa letu likabadili mwelekeo ikaanza mikakati ya kutetea haki za wanaume.

Upvote
1