DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
"Katika nchi hii sasa hivi mafisadi sio wanapiga kidogo wanapiga kiuhakika ni walaji na ni walafi na wanafanya vitu kama vile wananchi wa sasa hivi hawana elimu, lazima tufahamu sasa hivi ukienda sehemu yoyote hata kama ni kwenye kijiwe cha bodaboda utamkuta mtu wa chuo kikuu, utamkuta wa 'form six', utamkuta 'form four"
"Utamkuta wa darasa la saba na asiesoma wakikaa pamoja pale wakianza kuongea wote wanakuwa wapo chuo kikuu kwahiyo hawa watu sio kwamba hawaelewi mambo utakuta mtu yupo serikalini ana GPA ya 2.5 na mwendesha bodaboda ana GPA ya 4 "
"Sheria za TAKUKURU kama zimelegea walete tuzibadilishe watu kila sehemu wanajenga majumba watu wanaona tunapozungumza mambo ya leo tujue kuna 2030 inakuja tutakwenda kwenye chaguzi zetu"-Ahmed Shabiby, Mbunge wa Gairo, leo Januari 28, 2026.
Ameyasema hayo Bungeni, Ikiwa ni baada ya siku tatu tokea Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba alipowapongeza TAKUKURU kwamba wanafanya kazi kubwa katika kuthibiti Rushwa nchini.