Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa Mkoani Geita.
"Kituo cha Polisi kilichopo kipo katikati ya makazi ya watu na maeneo ya biashara habari njema ni kwamba IGP alituma timu yake hapa walishafanya tathimini hivyo mnajengewa Kituo kipya cha kisasa na mnapatiwa Wilaya ya Kipolisi hapa Katoro," alisema.
Aidha, Sillo amewahimiza Polisi kata nchini kuendelea kutoa elimu ya Polisi jamii kwa Wananchi na Viongozi wa Serikali za mitaa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na kutokomeza uharifu unaojitokeza maeneo mbalimbali ikiwemo wizi wa mifugo unaotajwa kuwepo kwa wingi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
"Wananchi mnapata taarifa za wezi, mnakaa nazo na wengine kuishi nao naomba toeni taarifa kwa Jeshi la Polisi ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Sillo.