KATUMBI AREJEA TP MAZEMBE

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
- Miamba wa Soka kutoka Nchini DR Congo, Klabu ya TP Mazembe rasmi imetangaza kuwa Rais wa Klabu hiyo, Moïse Katumbi Chapwe amerejea katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka Mitatu akikimbia adhabu ya kifungo kwa sababu za kisiasa.
:
- Tangu mwaka 1997, Katumbi amekuwa Raisi wa klabu ya TP Mazembe yenye maskani yake jijini Lubumbashi.. Miamba wamekuwa bora Kimataifa wakishinda Ubingwa wa CAF Champions League mara tano (ikiwemo Mara tatu za mwisho 2009, 2010 na 2015), CAF Confederation Cup Mara mbili 2016 & 2017 na Mabingwa wa CAF Super Cup mara tatu: 2010, 2011 & 2016; Mazembe Pia ilikuwa klabu ya kwanza kutoka Afrika kucheza fainali ya Kombe la Dunia kwa Vilabu "FIFA Club World Cup" mwaka 2010, wakipigwa na Inter Milan.
:
- Rais mpya wa DR Congo FelixTshisekedi ambaye amekuwa akihudhuria mechi za Ligi na za Kimataifa nchini humo, ikiwemo ya TP Mazembe na Simba SC ya Tanzania ,ametangaza maridhiano ya kisiasa na makundi mbali mbali nchini humo na adhabu ya kifungo cha Katumbi imetenguliwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…