Katuni (catoon)zinamwaribu mtoto wangu

Katuni (catoon)zinamwaribu mtoto wangu

kuchangumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
724
Reaction score
290
Salama wakuu!

Mimi nina mtoto wa miaka 5, mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka
na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe

Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni

Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?

Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?

Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu
 
Duh! kwangu kuna mtoto akiamka tu lazima aangalie katuni, tena yeye anaamka saa 12 kasoro utasikia anasema...."Tuni" ujue ndio katuni, au anasema jeri ujue ni katuni ya Thom&jerry,
Watoto wanapenda sana katuni kwani zinawafurahisha ila isiwe anatazama kwa kupitiliza.
 
kwa mtoto wa umri huo ni vema ukamtafutia katuni zenye mafunzo yatakayomsaidia kukua kiakili
mfano katuni zinazoendana na kusoma, kuabudu Mungu nk
itamsaidia kuiga tabia njema toka huko!!!
 
Mkuu kama mwanao anaangalia Tom and Jerry hakuna tatizo isipokua asipitilize! Too much is harmful!

Mwenyewe hauna la kuniambia nisiangalie Tom & Jerry!!!!! Teh teh teh teh!
 
Afadhali...maana kuna watoto wnajua movie za kivita, kijsusi hadi XXX wakiwa na miaka minne tu
 
Mpangie Muda hata nusu saa kwa siku mara tatu yaani morning nusu saa, mchana nusu saaa na jioni nusu saa
 
Salama wakuu!
Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka
Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe
Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni
Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?
Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?
Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu

Ndio muda wake mwache aangalie tena muongezee na ile ya dora ina mafundisho yani dogo anakuwa kama yupo darasani
 
Hata kama anapenda katuni inabidi uanze kuweka sheria.

Mfano, unampa maswali 10 akipata 7/10 unamuwashia katuni kwa masaa 2 akipata chini ya hapo unamwashia kwa nusu saa tu.

Nadhani itaanza kumjengea umakini wa elimu
 
ni nzuri mie nina niece ambae hufanya same ila yeye amekua controlled na akiambiwa imetosha anaskia naamini ni normal kwa watoto, ila ni vema ukamlimmit, its not good for health mtoto anatakiwa afanye physical activities na hicho kitendo cha kulia ikizimwa tv ni wrong attitude (ukizingatia tiari ana miaka 5) mzazi inabidi uwork on that, mtoto aisje akaku overpower/kukuchezea.
 
Back
Top Bottom