Kanuni za Chama
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) (c) (d) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
Hapo tu kuna waliopewa taarifa kwa simu na bila kufafanuliwa makosa yao ili wapate muda wa kutoa utetezi.
Ukiendelea mbele...
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au la.
Katika wote hakuna aliyepewa mashitaka kwa maandishi wala nafasi ya kutoa utetezi wala taarifa ya msingi ya mamlaka ya nidhamu. Mpaka hapo mwenendo mzima wa kuwafukuza uanachama ukawa batili.
Ukiwa na swali jingine uliza.