KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Uchaguzi wa Serikali za mitaa ukiwa umemalizika kwa amani na utulivu na tukiwa tunaendelea kusubiri matokeo kwa maeneo ambayo matokeo bado hayajatangazwa, tutumie muda huu kuijadili kauli ya katibu tawala wa mkoa wa Songwe aliyotoa siku ya jana, ya kwamba '....watawakagua wino watumishi ambao hawakupiga kura...'.
Hii ndio tathmini yangu juu ya kauli hiyo:
Ni kauli ambayo ndani yake imejaa vitisho na ubabe. Kupiga kura mtu halazimishwi ila anashawishiwa na sio kazi ya katibu tawala kuwahamasisha watu kupiga kura ila ni ya viongozi wa kisiasa kama wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri na wengineo. kitendo cha katibu tawala kutumia kauli ya kibabe na isiyo ya kushawishi bali ya kulazimisha inaweza kutafsiriwa vibaya kama kutakuwa na utekelezaji wa kauli yake kivitendo.
Ni kauli ambayo inawalazimisha watumishi wa umma kushiriki siasa kitendo ambacho ni kinyume na maadili yao ya kazi. Hebu tufikirie mtumishi wa umma huyu alijiandikisha kituo A na kutokana na sababu mbalimbali katika mtaa aliyojiandikisha huyu mtumishi wagombea wa chama A pekee ndio waliofanikiwa kupita. maana yake ni kwamba mtumishi huyu akienda kupiga kura atajulikana ni wa chama fulani. Je katika namna yoyote haiwezi kumuathiri kazini kama wakuu wake wajijua ? Swala la pili kwenye hoja hii, kwa yule mtumishi ambaye hapendi mambo ya vyama, vipi kauli hii haitamfanya aichukie Serikali hii kwa muingiza kwenye siasa na uvyama.
Ni kauli ambayo haijaangalia masuala mengine kwa ukubwa. kutokana na majukumu mbalimbali za kiutumishi alishindwa kujiandikisha hivyo kwa sababu yoyote angeshindwa kupiga kura. Je swala hili liliangaliwa kwa umakini kabla ya kutoa kauli hii.
Ni kauli ambayo kwa namna au nyingine imeitafsiri vibaya kauli aliyotoa Rais juu ya kuweka mapumziko 27/11/2024 ili watu wakapige kura. Kauli ya Rais ilisimama katika suala la kiimani zaidi, kwamba kwa kura siku ya kupiga kura ilikuwa jumapili basi wakristo walikuwa hawapati haki ya kupiga kura, kama ikiwekwa jumamosi basi wasabato wasingepiga kura na kama ingekuwa ni ijumaa basi waislamu wasingepiga muafaka ukawa ni siku ya jumatano lakini kwa kuwa jumatano ni siku ya kazi basi akaifanya iwe mapumziko na sio kwamba imewalazimisha watumishi waende kupiga kura. hata jumapili nayo ni mapumziko.
katika kuipima kauli ya katibu tawala mkoa wa Songwe, naweza kusema inaweza kuichonganisha serikali, Rais Samia na watumishi wa umma kama kutakuwa na utekelezaji wa kauli hiyo kivitendo na hata kama kusipokuwa na utekelezaji basi kwa namna moja au nyingine watumishi ambao hwakupiga kura watakuwa wameumizwa.
Mhe.Rais tunaomba umuondoe Katibu Tawala mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda ili kudhibiti kauli za namna hii kwa viongozi wengine ambazo zinaweza kuichonganisha serikali na watumishi.