Kauli gani ya Mwalimu ilikua inakukera!!?

Powder

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2016
Posts
4,977
Reaction score
6,635
KAULI GANI YA MWALIMU ILIKUA INAKUKERA SANA ME NAMBA 1

1. Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale

2. Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe

3. Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako

4. Mkimaliza kuongea niambie niendelee kufundisha

5. Baba ako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo apa

6. Wengine apa wekuja kusindikiza wenzao tu

7. Bichwa kubwa ubongo nukta

Ongeza na zingine....
 
O level
James Magreth yupo wapi? Mbona leo hajaja? (Magreth alikuwa jirani yangu ila sikuwa najua ratiba zake)
James huwezi kupata B ya somo langu...ukipata ntaandamana peke yangu.....

A. level
Niuzieni vitabu vyangu
Ukipata C yangu necta una A

Siku wakaja wakaguzi kutoka Halmashauri wakamuuliza maswali sijui lesson plans sijui nini akawaambia vitu vyote ninavyo kichwani akawaacha akaendelea kupiga pindi....

college
1. Huu muda unaoupoteza sasa utakuja mwakani....( alimaanisha Carry over)
2. Siwezi kufanya mua mkongojo ( Alimaanisha wasichana wa mwaka wa kwanza)
3. Umetafuta maksi 2 kwa miezi minne ukaikosa unataka mi nikupe kwa dkk 10 ntaipata wapi hebu fikiri hata ungekuwa wewe ( Aliwaambia wadai kozi weki).
 
Mm niliwahi kuulizwa


Unataka kuwa nani badae.?
Nikajibu 'rubani'
Mwal. akaniuliza, kwa akili ulizonazo unafikiri kweli utakuwa rubani.?

Ahhhhh 🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️ mamaeeeeeee kweli urubani nausikia kwenye tv tuu, sijui aliniloga fala yule 🤔🤔🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…