MpigaFilimbi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,169
- 187
WanaJF inaonyesha kuwa katika nchi hii kuna wakati au mazingira ambayo sheria inaruhusiwa kuvunjwa. Na kwa mantiki hii, basi kuna watu wapo juu ya sheria kama tunavyoshuhudia siku zote, lakini huwa haisemwi hadharani au haijaandikwa ila wahusika wanapractice. Nimekutana na hii kauli ya Lukuvi kama alivyonukuriwa na Majira kuhusu kuziachia daladala zisizo na leseni zioperate kuwapeleka watu kwenye sherehe za uhuru. Uhuru huo una maana gani kama mpaka sasa hatuwezi kufuata sheria?
Habari zaidi soma Majira
http://www.majira.co.tz/index.php?o...ksa-kesho&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57
"Siku hiyo magari yoye ya abiria yataelekea Uwanja wa Uhuru na nawaagiza Askari wa Usalama Barabarani, SUMATRA na Majembe Auction Mart kutoyakamata mabasi hayo, pia mabasi ambayo hayana leseni ya kusafirisha abiria ndani ya jiji hili, siku hiyo ruksa kufanya hivyo mwisho saa nane mchana," alisema.
Habari zaidi soma Majira
http://www.majira.co.tz/index.php?o...ksa-kesho&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57