MOSintel Inc
JF-Expert Member
- Mar 24, 2016
- 817
- 593
Wasalaam wakuu,
Poleni sana na shughuli mbalimbali za kujenga taifa.
Sote katika jukwaa la siasa tumekwisha shuhudia la mgambo likilia kwa vyama mbalimbali kuanza kampeni za uchaguzi wa tarehe 28, oktoba 2020.
Tayari vyama vimekwisha anza kunadi sera zao kupitia wagombea wao. Binafsi nimefurahishwa sana na ilani ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA. Kufurahishwa kwangu huko kumetoka na sera zao ambazo kiukweli zinagusa uchumi wa taifa letu(MACROECONOMICS) na pamoja na uchumi wetu sisi wananchi mmoja mmoja (MICROECONOMICS).
Sera za CHADEMA zenye fungamanisho la sekta ya umma na sekta binafsi (PPP or public-private partnership) ni nguzo katika kukuza uchumi wa nchi na uchumi wa watu wake.
Katika sera hizi mgombea wa CHADEMA nafasi ya Urais Mhe. Tundu Antipas Lissu ameanza kuelezea vyema utekelezaji wa sera hizi atakazozisimamia katika kipindi chake cha utawala wa miaka mitano( 2020-2025).
Sera hizi zimekwisha anza kupokelewa na watu wengi maana zinagusa kila kundi ikiwa ni pamoja na Wafanyakazi, Wakulima, Wajasiriamali, Wawekezaji, Wasomi na Wanafunzi wa elimu kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu.
Summary ya Sera za CHADEMA katika ilani yake ya 2020:
1. Katiba Mpya (ikiyasimamia maoni ya kamati ya Warioba)
2. Uhuru wa vyombo vya habari.
3. FAO LA KUJITOA LINARUDI
-ukiwa na utayari wa kusitisha mkataba wa kazi, utapokea mafao yako kulingana na mfuko wako mafao.
4. Maduka yasiyotozwa Kodi jeshini yanarudi.
5. Riba za mikopo ya elimu ya juu itashuka kutoka 13% mpaka 3%.
6. Sheria kandamizi zote zenye upendeleo kwa makundi fulani zitafutwa.
7. Maendeleo yatalenga watu na si vitu, kwamba ili nchi ipate maendeleo lazima kwanza watu wake waendelezwe kielimu(maarifa na ujuzi), kiafya na malazi(makazi Bora).
8. Kodi ya ongezeko la thamani VAT itakua 10% kutoka 18% ya Sasa hivi, ili kuchochea na kurudisha matumaini ya watu kurudi katika biashara na kuongeza uzalishaji mali na hivyo kuinua pato la Taifa.
9. Kodi ya ardhi itapunguzwa ili kuifufua sekta ya makazi ambayo katika kipindi hiki cha miaka mitano imefifia.
10. Kupandisha madaraja na mishahara ya wafanyakazi; swala ambalo lipo kisheria na litafanywa na serikali ya CHADEMA chini ya Rais wake Mh. Tundu Antipas Lissu.
11. Mazingira Bora ya uwekezaji. CHADEMA imepanga kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji ikitumia mbinu ya ubia wa sekta ya umma na binafsi katika kuwavutia wawekezaji kupitia punguzo la kodi na uendelezwaji, ufufuaji na uanzishwaji wa maeneo maalum ya kimkakati ya kiuchumi yaani SEZ(Special Economic Zones).
12. Matibabu kwanza malipo baadae; Kupitia bima ya Afya kwa wananchi wote serikali ya CHADEMA imejiandaa kutoa bima kwa wananchi wote ili kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Afya bora katika muda wote. Hii itapunguza vifo ambavyo mara kadhaa vimesababishwa na wagonjwa kukosa fedha za matibabu kwa wakati.
13. Kodi ya wafanyakazi kwenye mshahara (PAYE) haitazidi 8%. Serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kutoza kuchukua kodi ya PAYE isiyozidi 8% ili kupunguza kodi kubwa ambayo ni mzigo kwa Wafanyakazi.
14. Masharti ya mikopo kwa Vijana itakua nafuu. Wanafunzi wa elimu ya juu hawata daiwa madeni yao waliyokopeshwa na HESLB mpaka pale watakapoajiriwa either katika sekta ya umma ama binafsi.
15. Upatikanaji wa Maji Safi na salama kwa gharama nafuu. Serikali ya CHADEMA ikishirikiana na sekta binafsi imejipanga kusambaza na kutengeneza miundombinu ya maji Safi na salama kwa ustawi wa Watanzania.
16. kuboresha miundombinu vijijini. Vijijini ikiwa ndiyo sehemu inayokaliwa na watu wengi ambao ni wazalishaji wa Chakula na malighafi kwa ajili ya viwanda, serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kuimarisha miundombinu vijijini ili kuunganishwa maeneo ya kimkakati ya uzalishaji malighafi shambani na bidhaa viwandani.
Nawasilisha haya machache.
#Mpiga-kura_huru
#Uchaguzi2020
#TUKAPIGE_KURA
#TANZANIA-AFRICA
#VISION2025
#AGENDA2063