MKOLA MLIMA
Member
- Dec 9, 2012
- 55
- 15
Jana wakati natazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha ITV nimemsikia Nape akiongea na wananchi wa kata ya Kiborloni mjini Moshi, alisema 'wanaounga mkono serikali tatu ni wahuni'. je kauli kama hiyo inapaswa kutamkwa kiongozi kama yeye, ambaye anatambua kuwa maoni yaliyotolewa ni ya wananchi.
kwa maana hiyo wananchi walitoa maoni ya serikali tatu ni wahuni?
Angalizo: kwa hadhi aliyokua nayo Nape anapaswa kuchuja na kupima kauli zake kabla ya kutamka mbele ya hadhara.