Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Albert Chalamila, akiwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa tofauti, alijipatia umaarufu kutokana na kauli zake tata na zingine ambazo mara nyingi ziliwaacha watu hoi. Akiwa katika Mkoa wa Mbeya, aliwahi kusikika akitoa agizo la kuchapa viboko wanafunzi walioteketeza mabweni, jambo lililozua mjadala mkubwa kitaifa kuhusu mbinu za adhabu shuleni. Aidha, alipokuwa Iringa alifunguka alivyokabiliana na kijana aliyevamia nyumabni kwake, huku Dar akidai kudhibiti Wizi wa Transfoma kwa kuwanywesha Wezi Mafuta ya Transfoma.
1. Tulidhibiti Wizi wa Transfoma kwa kuwanywesha Wezi Mafuta ya Transfoma
Chalamila hapa anasema vitendo vya wizi wa mafuta ya transfoma katika mkoa wa Dar es salaam vilikirthiri, hivyo ili kukomesha vitendo hivyo waliamua kuwa yeyote atakayekamatwa anafanya vitendo hivyo atanyweshwa mafuta ya transfoma na mpaka sasa hakuna wizi wa transfoma Dar es Salaam
2. Akiwa RC MBEYA, Chalamila alisema Bar na Makanisa Shindaneni, Bia inaongeza Kinga
3. Wakati akiwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati akizungumzia ujio wa Rais Samia kwa ziara ya kikazi aligusia suala la Wananchi kujitokeza na mabango mbele ya Rais na kuzua mjadala mitandaoni
4. Chalamila alivyozungumzia kauli ya kuambiwa mpenda mapenzi
5. Chalamila alivyodhani Rais akiwa madarakani kwamba hawezi kufariki, "Nilishika moyo wangu na kumuuliza mke wangu au nimekufa na hutaki kuniambia"
6. Kauli ya Pombe na Kazi
7. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alivyowacharaza fimbo wanafunzi
Soma, pia Kauli tata za RC Chalamila kwenye matamko mbalimbali nchini
1. Tulidhibiti Wizi wa Transfoma kwa kuwanywesha Wezi Mafuta ya Transfoma
Chalamila hapa anasema vitendo vya wizi wa mafuta ya transfoma katika mkoa wa Dar es salaam vilikirthiri, hivyo ili kukomesha vitendo hivyo waliamua kuwa yeyote atakayekamatwa anafanya vitendo hivyo atanyweshwa mafuta ya transfoma na mpaka sasa hakuna wizi wa transfoma Dar es Salaam
- Chalamila: Vibaka wafanywe 'skeleton' za maabara iwe fundisho kwa wengine
- RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani
- Albert Chalamila: Hiki kizazi ambacho kimepata divisheni 0 au 4 tunakiweka kwenye kundi lipi? Tunazalisha kizazi ambacho hakina tija kwa taifa