Mwenyezi Mungu anawalani na zaidi anawaonyesha ni wapi panahitajika kuwepo kwa askari kuliko Pemba ,halafu mi nawashangaa sana hawa walinzi wanaowekwa kwenye mabenki utamkuta mlinzi analinda na gobore ,ei jamani ndio nilimuona pale TRA Temeke Benki ipo kando ya ofisi hiyo ya TRA ,kule tra kama hela ni nyingi wanakwambia ukalipe hapo benki na urudi na risiti ,nilipoenda benki nikaona yule mlinzi kachoka ile mbaya ,nilivyohisi hata ile bunduki aliyoishika anaiona nzito ,yaani kidogo tu ningemvaa na kuchukua changu hapo benki ila ile bunduki aliyokamata sikuiamini kwani nayo ilikuwa ni zile zilizotumika vita kuu ya kwanza.
Jambo jingine pale Temeke kwenye hii benki iliyoibiwa nilishawahi kwenda kama mala tatu kufanya utafiti wangu na pia kutoa hela ,kile kibanda cha ulinzi utafikiria ni sehemu ya kulindia mpunga tena imetengwa kabisa na benki eti walinzi ndio humo wanakaa ,nafikiri wamekijenga kwa maboxi tu hakina kinga yeyote ya kuweza kupambana kama kutatokea uvamizi ,tena kwa nionavyo hao jamaa kumi na tano ni wengi sana kuvamia pale ,yaani makomandoo watatu tu walioshiba maziwa ya mama yao wanaweza kabisa kuiteka benki na kuchukua wanachokitaka tena bila ya kuua mtu hata mmoja.
Ikiwa kuna majambazi ambao wamo humu JF nawaomba wazidishe ustadi wa ujambazi kwa kuweka rekodi za kuiba bila ya kuua au kujeruhu mtu ,na huu ndio wizi stadi unaofanyika siku hizi huko nchi za nje ,hivyo wangejaribu kusoma kwa wenzao ambao wanaiba kwa style ya cinema ,hauliwi mtu ,hakwaruzi mtu ,watu wanavamia sehemu kubwa tu tena zenye ulinzi wa aina yake zikiwep[o kamera na sensor ,hivyo mambo ya kuiba mamilioni na kuuwa huwa hayazawadiwi zaidi ya kusema nchi imevamiwa maana kwa wizi uliotokea hapo Temeke inakuwa kama ulinzi wa nchi umekuwa under estimated na hivyo ukipima hali hiyo ya watu kumi na tano na njia zilizopo kama kweli akina Manumbu wamejipanga kuilinda nchi hii au mkoa huu na hujuma za aina hii basi majambazi hao hawawahi kutoka nje ya Temeke.
Polisi hawa akina Manumbu na Kovu wote ni wateja wa ujambazi maana kwa upande wangu kule kwa wao kujigamba na kutoa makelele kuwa siku za majambazi zinaisabika hakunifanyi nione kuwa maneno yao ni kweli na hayana uzezeta ndani yake.
Polisi wa kweli huwa wanafanya mipango yao kiaina na wanajua ni namna gani wanaweza kuufunga mji within a minute ,so baada ya kusikika milio ya risasi wangeweza kuwasiliana mara moja na kujua wapi pa kufunga njia za kuingilia na kutoka Temeke badala ya wao wote na vingunge wao kujikusanya lilipotokea tukio ,huo ni woga na kujificha ,hivi jamani mnaenda kwenye tukio wakati watu wanaondoka ? SI mtapishana nao njiani huku wanawacheka ?
Walioouonyesha viongozi hawa wa ulinzi ni uzembe wa mwisho kabisa ,hili halina ubishi kwa maana walijua kuwa walihitajiwa kuziba njia kuu za kuingilia na kutokea Temeke ndio pale mlipowasikia kuwa asikari wetu wanajua kujipanga sijui helikopta inawafuata ,huo ndio ukweli ambao walitakiwa wakubwa na wadoge waizingire Temeke kila pembe mbali kabisa na tukio ili kuidhibiti mianya ya kutokea.
Namaanisha pale baada ya kusikia milio na kuonyesha kuwa si ya kawaida wao badala ya kukimbilia kwenye tukio ilikuwa wajipange nje ya Temeke na aidha kuzuia magari yalioko kwenye mipaka ya kuingilia na kutokea Temeke ili kuwapa ugumu wa majambazi ambayo yapo mbioni kutoka nje ya Temeke ,hivyo kama kweli walikuwa wanawafuata kwa helikopta basi majambazi hao wasingetimiza hata kilomita mbili. na gari zilizotumika nazo zingeweza kubakia humo humo ndani ya Temeke labda iwe majambazi wamewekeza gari za kubadilisha na kwa kuwa njia zimefungwa in no time wangeonekana tu magari yalio kwenye harakati.
Wamesoma lakini hawakufahamu ,zidini kupeleka majeshi na mapolisi Pemba na Mwenyezi Mungu atazidi kuwalaani na kuwafelisha katika kila harakati zenu na juhudi zenu ziwe hazizai matunda yeyote yale zaidi ya hasara ,mwenye kudhulumu hazidishi zaidi ya hasara ,askari hao wamevunjwa miguu ,kumbe nanyi mnaumia ?