Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema ameamini Ekaristi takarifu inaponya na inaleta undungu, kufuatia kitendo cha Padri Dkt. Charles Kitima kuwakutanisha pamoja Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, Tundu Lissu na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ambapo Chalamila amesema inawezekana hata yale mengine yaliyopangwa yakaahirishwa kwenye madhabahu.
Chalamila amesema hayo leo September 15, 2024 katika Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaaam.
“Ndugu yangu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Ndugu yangu, Baba yangu Emmanuel Nchimbi, kwakweli nimeamini Ekarisiti Takatifu inaponya na inaleta undugu, na inawezekana hata yale mengine yaliyopangwa yakaahirishiwa hapahapa kwenye madhabahu hii” —— RC Chalamila
Ingawa RC Chalamila hajaweka wazi kuwa ni mambo gani anayosema yanaweza kuahirishiwa kwenye madhabahu lakini Watu wanaofuatilia siasa za Tanzania wameitafsiri kauli yake kuwa huenda anazungumzia maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA September 23,2024 na kwamba huenda Chalamila anamaanisha kukutanishwa kwa Viongozi hao kunaweza kupelekea maamuzi ya maandamano hayo kuahirishwa.
Pia soma: Tutaandamana kwa sababu ni halali, Polisi wawachukulie hatua hao wanaosema watavunja amani