Kauli ya Mch. Mtikila kuhusu katiba mpya hii hapa

Kauli ya Mch. Mtikila kuhusu katiba mpya hii hapa

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
4,315
Reaction score
309
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema Chadema ilikurupuka na kudandia hoja ya Katiba mpya ya nchi bila kuzingatia maslahi ya Watanzania na kuonya kuwa mchakato wa kuunda Katiba unaweza kushindwa kama utafanywa kwa lengo la kukidhi matakwa ya watu wachache wanaoshinikizwa na wageni.

Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.

“Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa, jambo ambalo lilisababisha kampeni ya kutaka Katiba kuwa ngumu na isiyo na mafanikio … sasa watu hao hao wanataka Katiba mpya kwa maslahi yao,” alisema.

Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati.
 
uko sawa mtikila cha msingi ni watanzania kupata katiba itakayokidhi mahitaji ya watanzania na pia kwa nyie wanasiasa wa upinzani kusiwepo na kusemana tena ni wewe mtikila kukaa na viongozi wa vyama vingine na mkajiwekea mkakati mzuri wakutoa ushauri wenu juu ya kupata katiba mpya
 
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema Chadema ilikurupuka na kudandia hoja ya Katiba mpya ya nchi bila kuzingatia maslahi ya Watanzania na kuonya kuwa mchakato wa kuunda Katiba unaweza kushindwa kama utafanywa kwa lengo la kukidhi matakwa ya watu wachache wanaoshinikizwa na wageni.

Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.

"Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa, jambo ambalo lilisababisha kampeni ya kutaka Katiba kuwa ngumu na isiyo na mafanikio … sasa watu hao hao wanataka Katiba mpya kwa maslahi yao," alisema.

Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati.

Itamchukua muda mrefu sana NYANI kuona kundule...........
 
Nataka mtikila ajue kuwa kila jambo lina wakati wake. Kama yeye alidai na hakikutokea kitu au serikali haikujali, basi ajue kuwa muziki wa chadema ni sterio zaidi yaani unasikika zaidi. Mimi nitarajia mtikila angepongeza jitihada za cdm kupaza sauti kudai katiba. Huyu mchungaji ana misimamo ya ajabu ajabu tu, simshangai sana.
 
ndio maana tarime alipigwa mawe kwenye msiba wa chacha wangwe. Asilete unafiki wa kudai yeye ndio chanzo cha katiba mpya, profesa baregu kwa zaidi ya miaka 10 amekua akiongelea mapungufu ya katiba hii katika mihadhara yake,sasa anachostahili kufanya huyu mtikila ni kutuliza munkari wake na kushirikiana na wanaharakati wote kufanikisha azma hii inatimia. NB.hivi huyu mchungaji mtikila kweli ni mchungaji wa kanisa?na kama ndio nitashkuru kama nitajulishwa jina la kanisa lake na mahala lilipo, asanteni sana.
 
Anaomba kazi kwa Rais, good nafikiri ni vizuri akawa member mojawapo katika tume...siyo mbaya sana
 
Mchungaji mtikila ni mtu asiyetabirika na mara zote anaangalia namna ya kupata maslahi kutokana na hoja mbalimbali. Ameanzisha hoja nyingi sana nchini kuanzia Magabachori hadi wazawa lakini hazina nguvu wala mishiko sahihi kwa wachambuzi wa mambo. Huwa anaanza vizuri lakini anakorofisha mahali fulani huko njiani kabla ya kufika. Akiwa kama mtanzania anayo haki ya kuchangia uundaji wa katiba mpya lakini si mtu wa kumwamini kuwa ana nia ya dhati ya kusaidia watanzania. Tarime walimpiga mawe kwa usaliti wake!!!
 
ndio maana tarime alipigwa mawe kwenye msiba wa chacha wangwe. Asilete unafiki wa kudai yeye ndio chanzo cha katiba mpya, profesa baregu kwa zaidi ya miaka 10 amekua akiongelea mapungufu ya katiba hii katika mihadhara yake,sasa anachostahili kufanya huyu mtikila ni kutuliza munkari wake na kushirikiana na wanaharakati wote kufanikisha azma hii inatimia. NB.hivi huyu mchungaji mtikila kweli ni mchungaji wa kanisa?na kama ndio nitashkuru kama nitajulishwa jina la kanisa lake na mahala lilipo, asanteni sana.

Obvious hakuwa peke yake, bali naye ni miongoni mwa watu wa mwanzoni kabisa kuanzisha madai ya katiba mpya hapa nchini.
 
cHADEMA WAMERUKIA MKUKI KWA MBELE

CHAMA CHA KUIBA AGENDA ZA WENGINE NA KUZIGEUZA KUWA ZAO

SASA WANAADHIRIKA
 
mtikila ni fisadi hastahili kabisa kuwepo katika Tume ya Katiba. Kama mtakumbuka alishawahi kuumbuliwa na Rostom Aziz kuwa naye Mtikila huenda kuchukua hela ya ufisadi toka kwa RA, na hadi leo hajapinga! Mchungaji haaminiki bora apotezewe tu
 
cHADEMA WAMERUKIA MKUKI KWA MBELE

CHAMA CHA KUIBA AGENDA ZA WENGINE NA KUZIGEUZA KUWA ZAO

SASA WANAADHIRIKA

Inaonekana umeamka kutoka usingizini baada ya kubwishwa jana na mafisadi. Unaonaje ukienda 'kuchimba dawa' kidogo halafu ndiyo uchangie hoja?sijui unajua hata maana ya kudandia? Kama ndivyo, basi akili yako haina akili.
 
Tatizo ninaloliona hapa ni mfarakano wa vyama hivi vya upinzani, woote wana lengo moja na unapozungumzia katiba mpya marekebisho yake yako so obvious hata mtoto mdogo anaona!

Kindly,guys out there please someone wake up join up forces hii ya chadema kadandia, mara mimi ndio mwanzilishi, mara eti NCCR wanayo miaka mingi, mara , mara hazisaidii kitu chochote kile!

All in all, chadema wanalaumika kuwa ndio walioleta mifarakano ya umoja baada ya kupata wabunge wengi!!

kazi ipo ushabiki hausaidii kitu katika hili.
 
cHADEMA WAMERUKIA MKUKI KWA MBELE

CHAMA CHA KUIBA AGENDA ZA WENGINE NA KUZIGEUZA KUWA ZAO

SASA WANAADHIRIKA

Wote wanaomfanya Mtikilia kuwa mtu wa maana nao hawana maana! Sioni iwapo Chadema wanaadhirika chochote hapa. Kama ni hivyo basi, hata CUF na NCCR etc. Kwa nini iwe Chadema tu ndiyo wanaadhirika?
 
cHADEMA WAMERUKIA MKUKI KWA MBELE
CHAMA CHA KUIBA AGENDA ZA WENGINE NA KUZIGEUZA KUWA ZAO
SASA WANAADHIRIKA

Hivi hii issue ni ya CHADEMA au ni sisi wananchi wote???, au walikwambia wanataka Katiba yao peke yao kwa manufaa yao pekee??
 
Samahani alizungumza na nani ? Source..... Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.
"Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa,
Nijuavyo yeye alitaka marekebisho tu ya Mgombea binafsi akimtumia wakili Rweyongeza wa dodoma na akashinda mbele ya Jaji Mwalusanya (The Late) na ile Hoja ya Tanganyika.
wote wana manati na wanamlenga ndege, aliyemuangusha ni nani na aliyemkurupusha ni nani si wote wana nia moja katika suala la Katiba mpya au Marekebisho ya Katiba
 
Hivi swala ni nani kaanzisha mjadala au swala ni nini kinatakiwa? sijaelewa!
 
Back
Top Bottom