Bonson
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 183
- 147
Ndugu wana JF,
Kauli ya Waziri Wasira kama ilivyoandikwa na gazeti la RAI inaniongezea maswali lukuki kuhusu mchakato mzima wa katiba na umakini wa viongozi wetu. Kwa alichokisema ni kwamba hadi sasa rasimu ya Katiba Mpya bado haijafika kwenye meza ya Mheshimiwa Rais.
Cha kushangaza na kusikitisha na kinachonipa maswali ni kwamba Mheshimiwa Rais aliwezaje kulizungumzia swala la Katiba katika hotuba yake ya mwezi bila kuisoma au hata kuiona nakala ya Katiba yenyewe?? Je, muheshimiwa anawezaje kusimama mbele ya mamilioni ya raia wa Tanzania na kutoa msimamo kwa rasimu ya Katiba ambayo hajaiona wala kuisoma??
Utata mkubwa zaidi ni ujasiri alionao Mzee Wasira kwamba Katiba ikitua tu mezani, Mkuu ataweka saini yake na kuipitisha. Yaani Wasira hatoi nafasi kwa Rais kuisoma na kutoa msimamo binafsi. Hii ni kumuweka Mheshimiwa Rais katika pressure isiyo ya lazima. Kauli ya Mzee Wasira inahitaji ufafanuzi; Nanukuu kauli yake ; Ninachofahamu muswada ukija Rais atasaini kwa sababu taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini kama wenzetu wanahitaji kumuona Rais ni sawa, na amesikia wito na amekubali. Tusubiri matokeo ya mazungumzo. (mwisho wa kunukuu).
Mzee Wasira hakuisikia hotuba ya Rais akisema kwamba Zanzibar haijashirikishwa vya kutosha?? Hivyo basi utaratibu wote haukufuatwa!!
MUNGU IBARIKI AFRIKA; MUNGU IBARIKI TANZANIA!