Kauli ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam ni Dharau, Inachochea Machafuko, Badala ya Kuomba Radhi Anawatisha Wananchi” ✅

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Ni muhimu serikali iache kiburi. Kuomba radhi ni ishara ya uungwana na uwajibikaji, siyo udhaifu. Badala ya kutisha wananchi kwa kauli za kupiga na kuwavunja miguu, viongozi wanapaswa kutafakari: vipi iwapo polisi wakiwapiga wananchi nao wakaamua kupigana nao? Hayo matamshi siyo ya hekima, ni ya fedheha.

Mkuu wa Mkoa ametoa kauli ya ajabu, akidai anaweza kumpiga mwanaume mwenzake kana kwamba Watanzania hawana heshima au haki. Watanzania si walemavu, si viumbe wa kunyanyaswa. Wananchi hawa ndio wanaolipa kodi na ndio wenye nchi. Kwa nini wao ndio waumie, kupigwa, kutekwa au hata kuuliwa na vyombo vya dola bila kosa la msingi?


Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi Umehujumiwa Hadharani

Mradi wa mabasi ya mwendo kasi ulianza vizuri, ukiwa faraja kubwa kwa wananchi wa Dar es Salaam. Lakini mafisadi waliuhujumu hadharani. Walianza kukusanya pesa na kulisha matumbo yao bila kuongeza idadi ya mabasi, bila kufanya service, na bila kujali uendelevu wa mradi.

Matokeo yake ni fedheha: mabasi mengi yameharibika na yamejaa kwenye yadi, na sasa yaliyosalia barabarani ni mabasi sita (6) tu, ambayo hayawezi kabisa kuhudumia mahitaji ya mamilioni ya wananchi.

Fedha za mradi huu zimeishia mikononi mwa wachache, lakini hakuna aliyechukuliwa hatua wala kufikishwa mahakamani. Badala ya kuwawajibisha wahujumu wa mradi, serikali inawageukia wananchi wanaolalamika kwa vitisho na mabavu.


Polisi mnayoyatumia mabavu, mjue kuwa mabavu hayaleti suluhu. Ikitokea wananchi wakajibu kwa kupigana, hali itakuwa mbaya zaidi. Badala ya vitisho, busara inatakiwa.

Tunasisitiza: Mkuu wa Mkoa anapaswa kuchunga kauli zake, aache kuongea kwa kiburi, na kama hakuwa na utulivu akiongea (labda akiwa amelewa au amekosa staha), basi ni vyema akaomba radhi kwa umma.

Kiongozi bora ni yule anayejua kujinyenyekeza kwa wananchi wake, siye anayetumia mabavu na man
eno ya kuwadhalilisha.
 
Chalamila amekuja Dar. Ametukuta na ataondoka na kutuacha na jiji letu.

Hana lolote Chalamila, alipokuja alisema atatokomeza umalaya, kiko wapi, apite Mwananyamala nyuchi zinauzwa kuanzia saa mbili asubuhi, aje Buguruni bei ya malaya iko chini ya bei ya soda.

******* ndio wameongezeka mara dufu kwenye kipindi chake na anajua walipo na wanapouzia na wanao wauzia utamu.

This is Dar is a slum.
 
Duuuuh
 
Mlioko karibu na Chalamila, mshaurini anunue simu ya touch aachane na kiswaswadu alichotoka nacho shamba, kisha awe anaingia jf angalau mara moja kabla ya kwenda kulala. Atajifunza mengi lakini pia atajifunza kwamba mikwara haisaidii.
Aige mfano wa the BEST DAR RC MHESHIMIWA KANDORO (rip).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…