Kauli ya mulugo kwa waliokosa mkopo

pelanya

Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
21
Reaction score
5
Kaul aliyotoa naibu wazir wa elimu juu ya wanafunz waliokosa mkopo inaonyesh ni kiasi gani viongozi wetu ni vichomi mulugo amesema kasungula kalikuwa kadogo ivyo kila mtu auze alichonacho kama mbuzi kuku ngombe nk ili agaramie masomo kiongozi kama huyu kwa kauli zake hafai duniani na hata mbinguni mbona watoto wao wanapata mkopo tena wanaenda kusomea nje kwa mikopo ya board kw nini wao wasiuze magali yao ili na sis tusome mungu awape wepesi wote waliokosa mkopo 2013/14
 
hao wanafunzi washakuwa watu wazima..NDIO WATAMBUE UMUHIMU WAO UKIFIKA WAKATI WA UCHAGUZI
 
Sometimes wanaongea kama vile wanaishi sayari nyingine. Kumgharimikia kijana mpaka asome tuseme miaka 3-4 utauza kuku wangapi kwa kila kuku sh. 5,000 kwa maisha ya kijijini au mbuzi wa sh. elfu 20 mpaka 50 kwa maisha ya kijijini, au ngo'ombe wa laki mbili kwa maisha ya kijijini. Anaongelea mfugaji gani wa kuwa na kiasi cha kufikisha let say 2milioni.
Ni mkulima gani wa mahindii, ndizi, kahawa, pamba, korosho, nazi mazao yanayokuja kwa msimu mmoja kwa mwaka auze ili amsomeshe kijana huyo na chuo na wadogo wake sekondari, na uku nyumbani wakinunua mafuta ya taa na chumvi?[
QUOTE=pelanya;7521403]Kaul aliyotoa naibu wazir wa elimu juu ya wanafunz waliokosa mkopo inaonyesh ni kiasi gani viongozi wetu ni vichomi mulugo amesema kasungula kalikuwa kadogo ivyo kila mtu auze alichonacho kama mbuzi kuku ngombe nk ili agaramie masomo kiongozi kama huyu kwa kauli zake hafai duniani na hata mbinguni mbona watoto wao wanapata mkopo tena wanaenda kusomea nje kwa mikopo ya board kw nini wao wasiuze magali yao ili na sis tusome mungu awape wepesi wote waliokosa mkopo 2013/14[/QUOTE]
 
Viongoz wote wa nchi hii wamezaliwa na mama mmoja kutokana na kufanana kwa kauli zao kwa kejeli,,,,,,wanajua hamtawafanya kitu,polen sana wadau mlokosa mkopo
TUREJEE KAULI ZA BAADHI YA VIONGOZI
1.pigeni,tumechoka
2.watakaoshindwa kulipia panton wapige mbizi
3...........
 
Wacha niamini kua naibu waziri huyu ni mvuta bange. Kwanini nasema hivyo? kati ya tabia za hovyo za mvuta bange ni kuropa chochote tu ili mradi ndicho kilichopo mawazoni mwake kwa muda huo.
 
Jamani leo tumerudi tena kwa wazir mkuu,kiukweli hatjapata jibu lolote la msingi zaidi ya kufukuzwa na walinzi pale getini,kwa waziri mkuu.Kama kawaida ye2 hatukukata tamaa baadhi yetu tukaelekea kwa mkuu wa nchi(IKULU),Tumeambiwa kesho turudi saa nne hasubuhi.ktakachojil ntawafahamisha.
 
EBANA MUNGU AWATANGULIE MAANA TUKO KWENYE KILIO KIMOJA.WENGINE TUKO MBALI SANA NA JIJI KUWEZA KUWAONA HAO WAKUU, TUNAWAUNGA MKONO KWA NJIA YA SALA NA IMANI.:amen:
 

Huyu bwana hafai hata kuwa kiongozi wa nyumba kumi. How could he say that to these kids? Tena waziri mwenye dhamana ya elimu? Waende wakauze nini hawa vijana? Eti hao ndiyo washauri wa rais. Watamshauri nini watu ambao hawawezi kuwaza? Big Results Now. Let's wait and see.
 
Mulugo akili yake haizidi ukubwa wa punje ya ulezi. Tunaomfahamu vizuri hatushangai uduni wake wa fikra na utendaji hovyo usio na tija hata tone moja kwa nchi hii. Kumweka huyu maamuma kwenye nafasi kubwa na muhimu sana kwa taifa hili na vizazi vijavyo inawezekana siyo bahati mbaya. Ni moja ya mbinu za kudumaza uwezo wa watanzania ili waendelee kuwa kama misukule kwa manufaa ya biongozi wachache ambao watoto wao wamesomeshwa na wanaendelea kusomeshwa nje ya Tanzania kwa fedha za walipa kodi, na pia kwa manufaa ya mataifa yaliyowaweka madarakani. Mwisho wa taifa lolote huanzia pale maarifa na ufahamu unapoanza kwisha au kudumazwa. Siyo ajabu kuona kuwa wote waliokosa mikopo ni wale ambao hawakuwa na fedha za kuwahonga wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ambao wengi wao pia walipata ajira zao kwa kutoa rushwa au kwa vimemo. Wafanyakazi wa Bodi wamefikia hatua ya kuweka mawakala wa kuchukua rushwa toka kwa wanafunzi wanaoomba mikopo. Hali hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii iliyostaarabika kama ya Tanzania.

Hakuna namna yoyote ambayo jambo hili linaweza kuvumiliwa. Rushwa, upendeleo na kujuana ni vitu vya kupigiwa kelele na kupigwa vita na yeyote mwenye akili timamu na uzalendo wa kweli kwa Taifa hili.

Wote mliokosa mikopo SIMAMENI HIMA NA KUWENI IMARA kudai haki yenu hadi mpate. Pigeni kambi nje ya Ofisi za Bodi mkifunga, kulia na kusaga meno bila kufanya vurugu.

Wakizima macho, masikio na akili zao, msiishie hapo. Waombeni wanaharakati na wazalenfo wengine kuwaunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…