Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kabla ya kauli ya Raisi coolidge,mtangulizi wake aliwahi kusema kwamba "binadamu wote ni sawa" lakini kauli hii ina mapungufu mengi sana na inaweza kupata ushindani mwingi.
Lakini maneno ya Raisi Coolidge bado yanaishi mpaka leo,na ndio msingi wa mafanikio yoyote yale duniani,alisema hivi "kuwa na malengo madhubuti au maamuzi madhubuti na kudumu nayo ndio msingi wa mafanikio yoyote yale hapa duniani"
Ndugu zangu hakika ni kweli kabisa ili tufanikiwe katika nyanja yoyote katika maisha yetu basi hatuna budi kuwa na malengo ambayo ni imara na kisha tuhakikishe tunayadumisha ili hatimaye tufikie kule tunapotaka kufika,mathalani umeweka lengo la kufanya biashara ya mazao basi huna budi udumu katika lengo hilo pasina kuyumbishwa na mtu yoyote yule au kuyumbishwa kutokana na changamoto mbali mbali,kwa kufanya hivyo hakika utafika kule unapotaka kufika.
Kipaji pekee hakiwezi kukufikisha kule unapotaka kufika kama huna malengo madhubuti na ukadumu nayo na kutimiza ndoto zako,wale ambao hufika mbali ni wale ambao wanaendelea kufanya jambo lilelile kwa miaka nenda miaka rudi bila kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile
Natamani wanafunzi na wanachuo watambue toka mapema kabisa katika maisha yao kwamba determination na persistance ndio kila kitu katika maisha,bila kuwa na hayo mambo mawili ambayo ni muhimu kabisa basi kila utakalo lifanya ukipata changamoto kidogo hukawii kukata tamaa.
Lakini ukidumu na mambo hayo hakika iwe mvua iwe jua utaendelea kupigania ndoto zako na mwisho wa siku utaona mafanikio yake,mfano ni Michael Jordan, alikuwa na nia ya kuwa mwanakikapu bora,pamoja na kukatiliwa katika timu ya shule lakini bado aliamini katika malengo yake na kudumu nayo,pamoja na kukosa mitupo mingi ya basketball lkn aliamini katika ndoto zake,na leo hii ameacha heshima kubwa kama mwanakikapu bora hapa duniani
Henry ford mwanzilishi wa magari ya ford,kipindi fulani alipambana sana kutengeneza gari lenye six cylinder,ilikuwa ni ngumu sana na watu walimkebehi lkn ilichukua mpaka mwaka mmoja kwa mafundi wake kufanikiwa kutengeneza gari ya namna hiyo,kila mara mafundi wake walipo mjia na kumwambia haiwezekani,aliwaambia endeleeni kufanya mpaka tufanikiwe,na hatimaye alifanikiwa.
Hii balbu au glopu ambayo tunawasha taa kiurahisi tu leo hii,mpaka hapo ilipofikia,yalipita takribani majaribio elfu moja mpaka kuwa na balbu ambayo leo tunayo,siri ni kuwa na malengo na kudumu nayo
Naweza kutoa mifano mingi sana hapa, lakini itoshe kusema siku zote kuwa na malengo madhubuti kisha ishi nayo na dumu nayo hakika utafika pale unapotaka kufika.
Ni hayo tu!