Kauli ya "Rais katoa hela" ni sahihi kwa kiasi gani?

Kwenye Political science, hicho kinachofanyika kinaitwa ' Propaganda' ili kum-brand Kiongozi na aweze kupata Political mileage mwisho wa siku lengo la yeye kupata nafasi nyingine ya kuchaguliwa liweze kutimia. Kila kiongozi hadi Mtendaji wa Kijiji analazimika kusema hivyo...
 
Wanaamini kuwa Watanzania wote ni wajinga hivyo hawajui kuwa hizo ni fadha zao na si za mwanasiasa yeyote?
 
Wanaamini kuwa Watanzania wote ni wajinga hivyo hawajui kuwa hizo ni fadha zao na si za mwanasiasa yeyote?
Jambo likirudiwa mara nyingi, jambo lile lile huwa kuna hali flani hivi ya kuonekana ni jambo la ukweli. Jambo hilo litajiumba na mwisho wake linapata nguvu. Unadhani ni kwanini viongozi wa nchi nyingi zenye demokrasia ya kuunga unga huwa wanafanya censorship ya habari? Na ukumbuke Afrika ni bara giza na wenye ufahamu kama ulionao bado ni wachache japo jana si kama leo. Tunapiga hatua kidogo..
 
Ni utapeli tupu, fedha ni mali za wananchi
 
Labda zinatoka kwenye mshahara wa mheshimiwa.
Teh! Ila kauli hii na ile ya kutoa "Utukufu" hua zina utata saana...
Utaskia "bunge tukufu"/"mapinduzi tukufu"....nadhani haya yangebakia kwa Mungu tu....ni vikauli vya ovyo ovyo saana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…