Kauli ya Rais Samia na Changamoto ya Rushwa Inavyoathiri Taifa: "Kuleni Kulingana na Urefu wa Kamba Zenu"

Kauli ya Rais Samia na Changamoto ya Rushwa Inavyoathiri Taifa: "Kuleni Kulingana na Urefu wa Kamba Zenu"

Gabeji

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1,530
Reaction score
1,903
Mheshimiwa Rais, nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pole na majukumu yako mazito ya kitaifa, kwani hakika mambo ni mengi na muda ni mchache.

Katika ngazi yoyote ya uongozi, ni muhimu sana kwa kiongozi kuwa makini na maneno anayoyatamka, hasa akiwa mbele ya watu. Kwa kawaida, ukitaka kumjua mtu vizuri, angalia maneno anayoyatoa. Biblia inasema kuwa "ndani ya ulimi kuna mauti na uzima." Watu wengi wamepoteza kazi kwa sababu ya maneno yao. Mfano mzuri ni Moses Nape Nnauye na wengine, ambao walikumbwa na matatizo kwa kutumia vibaya ulimi.

Kwa bahati mbaya, katika nafasi ya urais, inaonekana mara Rais anapotoa kauli, hawezi kuitengua. Sijui kama ni katiba, nafasi ya urais kuwa kubwa sana, au ni utamaduni wa Watanzania. Je, Rais hawezi kuomba msamaha mbele ya wananchi waliomchagua?

Hoja yangu ni kwamba, usilalamike hadharani kuhusu ukusanyaji wa kodi na kwamba mapato yanaingia mifukoni mwa watu wachache. Hapo awali, ulisema "kuleni kulingana na urefu wa kamba zenu." Kama sijakosea, hujawahi kutengua kauli hii, na kwa hakika imeathiri afya ya serikali yako, maana inaonekana kama umeruhusu rushwa.

Leo, nilitegemea ungetoa kauli ya kimamlaka kukemea wizi, rushwa, na ubadhirifu wa mali ya umma kuanzia mawaziri, wakurugenzi, TRA, na watendaji wakuu wa idara mbalimbali. Ingekuwa vyema kauli yako ya kuhalalisha rushwa iondolewe kwa vitendo na sio maneno tu.

Bila shaka, rushwa katika awamu hii imezidi awamu zote. Kila kona ya nchi imejaa rushwa, ufisadi, na matumizi mabaya ya madaraka. Umejaribu kupambana, lakini fedha bado zinaishia mifukoni mwa wachache, na deni la taifa linazidi kuongezeka. Kwa unyenyekevu mkubwa, nakuomba Mungu akupe nguvu siku moja ufute kauli yako ile kwa vitendo na ukemee rushwa kama kiongozi mkuu wa nchi. Taifa linaangamia kwa rushwa kana kwamba halina kiongozi wa juu.

Mawaziri wako wamekuwa mabilionea kutokana na rushwa, huku maisha ya wananchi yakiendelea kuwa magumu. Bei za bidhaa zinapanda, na pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho linazidi kuongezeka. Taifa letu limekuwa kama shamba la bibi.

Nisikuchoshe Mheshimiwa Rais. Mungu ibariki Tanzania.

Kwa heshima,
Mwinjilisti Gabeji

Pia soma:Rais Samia, hii kauli inazidisha ukakasi kwenye eneo la urefu wa kamba...
 
Back
Top Bottom