pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 282
- 561
Hongera/pole kwa majukumu, Rais Samia hongera kwa jitihada ulizoanza kuzionyesha kwa kipindi hiki ulichoshika madaraka vitu kama mahusiano ya kimataifa, uhuru wa vyombo vya habari, haki za binadamu na demokrasia ni baadhi tu ya mambo ambayo umeelekeza nguvu na kiukweli nikupe hongera katika hilo.
Leo nimekwenda kwenye afisi ya NSSF kufuatilia mafao yangu baada ya kustaafu kazi miaka mitano iliyo pita nilipofika nikaambiwa kuwa muajiri hajaweka michango yangu kwa miezi kumi.
Nikapewa fomu nimpelekee nilipofika nikakutana na afisa rasilimali watu akanieleza kuwa Tangu yule baba alipofariki mambo yamekuwa siyo kama zamani kwanza mishahara inapitiliza mwezi ukienda kuuliza unaambiwa nenda popote lakini wakati wa hayati RIP mishahara ilikuwa inatoka tarehe 25 na walikuwa makini kuhakikisha kuwa haki za wafanya kazi hazibakwi.
Nikamwambia yule afisa kuwa NSSF wamesema kama msiponiwekea michango yangu kwa miezi iliyobaki watatuma wakaguzi yule afisa alicheka mpaka alipaliwa akasema hawa hawaogopi chochote tangu hayati alipo lala na siku alipo lala walifanya sherehe kubwa sana.
Kumekuwa na maujanja janja mengi sana kwenye kodi na mifumo mingine ya uendeshaji ila mbaya zaidi ni pale wanyonge tunapominywa haki zetu kama kulipwa mishahara na stahiki zingine na hatuna pa kulalamika kwa kigezo kuwa tusiwabugudhi wawekezaji inauma sana.