kauli ya udhadhalilishaji dhidi ya kocha Mgunda nitafurahi sana endapo Ally kamwe atawajibishwa na Bodi ya ligi ili iwe fundisho kwa wengine.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kupitia sheria na kanuni zilizowekwa za Bodi ya Ligi kuhusu udhibiti wa viongozi huenda Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Ali Kamwe akafungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, endapo sheria zitafutwa baada ya kumfananisha Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda na Andazi mbele ya Mashabiki wa Young Africans.

Kwa mujibu wa Kanuni nambari 46 : udhibiti wa viongozi kifungu nambari 8 kinamfunga Ally Kamwe kwa maneno wa kashfa na dhihaka kwa Juma Mgunda, na mbaya zaidi aliyatoa hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari.

Kanuno hiyo inasema: “Kiongozi Akitoa matamshi au ishara za matusi dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, Klabu au Taifa atatozwa faini ya shilingi milioni moja 1,000,000/- na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3).
 
"E="Slim5, post: 46585862, member: 196493"]
Amepost Akiomba RADHI
[/QUOTE]Hata Manara alimuomba radhi Karia lakini rungu halikumuepuka. Sheria zifuate mkondo wake.
 
Amepost Akiomba RADHI
Dogo mpuuzi sana. Alianza kwa upuuzi wake wa kuandaa Tamasha la kuwacheka Simba kwa kuishia robo fainali badala ya ku mind business za Yanga.
Sasa hivi kanaleta ujinga mwingine. Mgunda ni muajiriwa, mtu rasmi kama yeye na kwa nafasi yake hapaswi kabisa kufanya such attacks
 
Yule Dogo Sikio limezidi kichwa baada ya Kutua YNG! Ni vile hana akili za kutafakari, angejiuliza wako wapi BUMBULI na NUGAZ
 
...ameomba radhi, lakini rudia kusikiliza alichosema Kamwe...Je amesema Juma Mgunda au Mgunda, na je kuna Mgunda wangapi Tz...
 
...ameomba radhi, lakini rudia kusikiliza alichosema Kamwe...Je amesema Juma Mgunda au Mgunda, na je kuna Mgunda wangapi Tz...
Unashupaza shingo kutetea ujinga
Sasa Kama siyo kocha Mgunda mbona kaomba radhi au kamuomba manara.
 
...ameomba radhi, lakini rudia kusikiliza alichosema Kamwe...Je amesema Juma Mgunda au Mgunda, na je kuna Mgunda wangapi Tz...
We jamaa vp ww? Acha kua na akili kisoda
Hivi ukimdhihaki kikwete hadi useme Jakaya mrisho?

Au inakuhitaji kusema John Joseph Pombe Magufuli ndio iwe umemdhihaki Magufuli?
 
...ameomba radhi, lakini rudia kusikiliza alichosema Kamwe...Je amesema Juma Mgunda au Mgunda, na je kuna Mgunda wangapi Tz...
Acha kujifanya huelewi. Ujinga hautakiwi kutetewa kwa namna yoyote ile. Uzuri TFF sio haifanyi kazi kama Mahakama.
 
Pale Azam walimtukana sana Kamwe pamoja na ujinga wake Mdemu aliopita nao kwenye magroup ya kazini wakawa wanadai hajakomaa kiakili mpaka makuzi yake.
 
Kumbe we jamaa ni mtu wa mpira haswa ,nimekujua km mtu unayeipenda sana yanga ila Leo untetea mtu wa Simba ,hakika we jamaa una utu sana .
Ifike hatua kwenye utu wa mtu ushabiki wetu ukae pembeni,hata msemaji wa Simba ana kimdomo sana bila kumsahau manara hata kipindi yupo Simba sijawah mkubali Wala kumwelewa .
Kipindi yupo Simba nilikua nampiga sana spana za wazwaz huko IG Hadi aliniblock mazima had Leo.
Kuna maisha baada ya mpira huyo dogo Kwa hiyo kauli kqzingua sana
 
Haji manara kaharibu sana mpira , usemaji wa mpira umekuwa wa ovyo sana ndio maana hawa akina kamwe na mwenzie ahmed wamekuwa wakiongea ujinga ,matusi, non fact etc...mimi hakuna siku ntafungua clip au etc nimsikie kamwe au Ahmed..mimi ni mshabiki wa simba lakini hakuna mtu ananivutia na napenda kumsikia kwenye mpira wa Tanzania kama Eng hersi..jamaa ana nidhamu sana ya kuongea..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…