Kauli ya Wizkid baada ya MTV EMA kumpokonya tuzo na kumpa Alikiba

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Hapo awali, Wizkid hakuwa mtu aliyejishughulisha kabisa na masuala ya tuzo. Lakini siku za hivi karibuni baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye MTV MAMA, huenda aliamua kuufungua moyo wake.

Na sasa kuna kila dalili kuwa akarejea tena kwenye msimamo wa awali wa kuzichukulia tuzo kama si kitu cha maana baada ya kudaiwa kuwa MTV EMA wamesitisha ushindi wake na kuamua kumpa Alikiba kwakuwa ni dhahiri kwa mujibu wa kura ndiye aliyekuwa akistahili.

Baada ya hilo, mashabiki wengi wa Alikiba wameivamia page yake ya Instagram na kumporomoshea kila aina ya maneno, mengine yakiwa yamejaa kejeli.

Huenda maneno hayo yalimwongezea hasira zaidi alizozipata baada ya kupewa taarifa hiyo mbaya kiasi cha kuamua kufuta post alizokuwa ameweka kwenye Instagram kusherehekea ushindi.

Kupitia Twitter, huenda akawa ameamua kutupa jiwe gizani na wengi wametafsiri kuwa ndio ‘reaction’ yake baada ya kutokea hayo.


 
hvi inakuaje unampa mtu tuzo alafu unampokonya huu ni udhalilishaji kabisha watoa tuzo wapaswa wajipange.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…