Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Naomba niweke wazi hapa nahitaji kueleweshwa juu ya hili suala. Katika hotuba yake Waziri wa mambo ya ndani alidokeza juu ya utawala ndani ya wizara ya Mambo ya ndani, akadai hana nyota na wala yeye si Amiri jeshi mkuu. (Hili nakubali asilimia mia). Hivyo ameonyesha wazi kuwa hatakuwa anamuingilia kiutendaji Mkuu wa Jeshi la Polisi. (Mimi ndio nimeelewa hivyo). Jambo ambalo linaonyesha mtangulizi wake alikuwa akimuingilia kiutendaji maana nimesikia kuwa alikuwa anaambiwa toa huyu weka huyu.
Lakini sheria inayosimamia shughuli za Polisi hapa nchini ( Police Force and Auxilliary Services Act) kifungu cha 7 (1)(2) kinaweka bayana kuwa IGP atafanya kazi kwa mujibu wa amri za Waziri . Kwa ufupi anaripoti kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Sasa basi nauliza tu je huyu jamaa aliyeondolewa alikuwa anafanya makosa kumpa IGP orders?
Nahitaji msaada ili nieleweshwe.