Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 444
- 488
Tuliamini na kuaminishwa kuwa kilimo ndio UTI wa mgongo wa nchi yetu.
Tafadhali Serikali tusiwatie watu wetu maskini mchanga machoni kwa kuchezea kilimo. Wakulima wengi ni hoehae, ambao ni Serikali pekee inaweza kuwakomboa. Hali ilivyo Sasa ni adaa na dharau kubwa kwa wakulima.
Kauli za kibabe zimekuwa nyingi katika pembejeo za kilimo kuliko uhalisia. Ni mabovu tuu ya watendaji badala ya kutafuta namba Bora ya kuliendea suala la pembejeo. Busara zimeondoka.
Eti mbolea ya ruzuku kwa tiketi!!! Na haionekani, tunakitafuta nini kwa wavuja jasho! Kwanini utaratibu uliotumika katika mafuta wa kuweka ruzuku huko usitumike kwenye mbolea na pembejeo za kilimo? Nani anapanga foleni kupata namba ya ruzuku ili aweze kununuwa mafuta?
Nashauri Serikali kulitazama hili zaidi ya inavyolitizama katika mafuta. Tunawatengenezea wananchi umasikini wa kutupwa na njaa itatamalaki.
Tujifunze kilichotokea kwenye Korosho. Pembejeo kucheleweshwa, kupatikana kwa shida na kutokidhi mahitaji hata ya mkulima mwenye heka moja.
Mhe. Raisi wetu shituka na kinachoendelea katika sekta hii adhimu yenye kundi kubwa la waathilika. Pamoja na mapungufu machache yaliyokuwepo katika awamu ya tatu na nne, lakini ni Bora mara Sabini. Tuboreshe utaratibu wa Dr. Kikwete na Mhe. Mkapa bila Soni.