Mwinjilist mtume nabii
JF-Expert Member
- Feb 21, 2015
- 2,437
- 1,097
Matatizo yako katika kila sekta na mafanikio pia. Kuna matatizo kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, elimu, maji, ajira, nishati, miundombinu na kadhalika. Kiongozi mzuri ni yule anayetambua mafanikio na kuyatumia kama msingi wa kupambana na matatizo yaliyopo. Wakati wote kutakuwa na matatizo. Maendeleo ni mchakato wa kutatua matatizo na ni mchakato wa kudumu. Hakuna nchi, hata zile ambazo zimeendelea sana, ambazo zimemaliza mchakato wa maendeleo na kumaliza matatizo yote
mgombea urais wa ccm magufuli mara nyingi amekuwa akiongea maneno ambayo mm naona kama anaipinga au kuishutumu serikali ya awamu ya 4 pale anaposema:
>nashangaa kuona akina mama wajawazito wanalala chini
>vijana hawana ajira
>wanafunzi hawana madawati nk.
je, hapo si kuonyesha kuwa rais jk hajafanya kitu??
ANATAKIWA ASEME HIVI:
>kwenye afya serikali imefikia hapa,na mimi nitafanya haya na haya
>kwny elimu awamu ya 4 imefikia hapa, na mimi nitafanya haya na haya.
LAKINI KWA JINSI ANAVYOONGEA MIMI KAMA MCHUNGAJI NAONA KAMA ANAJIKOSOA NA KUIKOSOA SERIKALI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Miaka minne baadae, CCM ni ile ileHayo mambo yote na zaidi ni matokeo ya kushindwa kwa hiyo hiyo CCM anayoiwakilisha na kuitumikia.
Nani anayeweza kuja hapa na kusema si CCM ambayo imeshindwa kuyatatua matatizo ya watu?
Leo hii tupo karne ya 21 lakini eti bado tuna wagonjwa wanaolala sakafuni mahospitalini na watoto wanaokaa chini madarasani na wengine hata kusomea chini ya miti!
Karne ya 21 bado tunahangaika na mambo ya mgao wa umeme!
Karne ya 21 kuna sehemu hapa hapa Dar maji ya bomba hakuna!
Halafu kuna wajinga bado wanaliona hilo li CCM kuwa ndo li chama la maana.