denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Kila nikijiuliza kwa nini Yamga wamefukuza benchi lao la ufundi kwa kupoteza mechi moja nakosa jibu, hii kitu naamini itamshangaza kila mpenda michezo duniani kote.
Wengi wetu hujidai makocha hasa mida ya jioni tukiwa kwenye vijiwe vyetu vya kahawa, huitoa timu kasoro hasa pale inapotoka sare au kupoteza mchezo, hatupendi kabisa kukubali ubora wa opponents wetu, sisi kila siku huamini timu zetu ni bora zaidi ya nyingine zote.
Hili pia huchangiwa na kauli za viongozi/wadhamini kuwajaza ujinga wapenzi wa timu zao, unakuta mdhamini anasema wazi timu yetu isipokuwa bingwa nilaumiwe mimi, hapa unajiuliza huyu mtu huu ujasiri wa kutoa kauli kama hii ameutoa wapi?
Kauli kama hiyo husababisha wapenzi wa hizi timu kusahau matokeo mengine kama kutoa sare au kufungwa, wao huamini timu yao sio ya sayari hii na lazima washinde kila siku kila mchezo hata kama ukiwa wa kirafiki, hatuwezi kabisa hata siku moja kukubali matokeo ya kufungwa timu yetu na kukiri opponent alikuwa bora zaidi, timu ikifungwa tu ataanza kutafutwa mchawi.
Kama hatupendi timu zetu zifungwe ni bora tutafute ligi ya nyumbani kwetu, tucheze na familia zetu, hapo watoto watakuwa waoga kumfunga baba yao, hivyo baba atakuwa anashinda tu kila siku, lakini kama tunaenda kucheza na wanaume wengine, nao wamefanya mazoezi yao vizuri kujiaandaa na mechi husika, ni vyema tujifunze kukubali ukweli.
Kufukuza kocha kwa kupoteza mechi moja ni ajabu, na hao wadhamini wawe wanachunga kauli zao, wasitoe kauli za kuwachanganya mashabiki wakaami timu yao inaundwa na malaika toka mbinguni, hili likifanyika litasaidia kupunguza pressure kwa wachezaji na makocha wao, na sisi pia tutaondoa ile tabia ya kuzimia uwanjani hasa siku hizi timu mbili kubwa zinapokutana pale Uwanja wa Mkapa.