Kauli za ney wa mitego ni ngumu kuliko za sifa. Sifa boniventure anaonewa. Aachiwe haraka.
Hivi hiki kiwimbo Cha sifa kina maneno mazito Kama nyimbo ya amkeni ya ney? Kama sio why ney yupo nje na sifa yupo ndani?
Tuachane na Hilo, twende kwa Lissu, Hivi kwa maneno ya lisu ukiyalinganisha na haya ya sifa boniventure yepi mazito?
Tuache kudeal na maswala ya kitaifa kwakuangalia umaarufu wa watu. Sifa boniventure aachiwe haraka ,na huu uonevu uishe haraka.
Cha kushangaza wamemnyima hata dhamana kana kwamba katenda kosa la uhaini wa kutaka kumuua Rais Samia Suluhu Hassan..!
Hawa watawala waoga sana. Wamejaa hofu na mashaka usiku na mchana. Wanaogopa na kukimbia na kutetemeshwa hata na unyasi unaotikiswa na upepo
Ndio maana sasa wanafanya matendo ya hovyo na kutumia njia zozote kujilinda wakifikiri wataepuka ghadhabu ya hukumu ya Mungu ambayo imekwisha kuwajia tayari...
By the way, wote
Ney wa Mitego na
Sifa Boniventure au Tundu Lissu na mwingine yeyote hawastahili kufanyiwa chochote, hawastahili kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa sababu tu ya kutumia jukwaa la kisiasa kutoa maoni Yao kuisema na kuikosoa serikali na Rais Samia Suluhu Hassan (Tundu Lissu) au kueleza yanayoendelea katika jamii kupitia Sanaa ya uimbaji ( Ney & Sifa)..
Hiki kinachofanywa na serikali kupitia chombo chao cha mabavu (polisi) kinaitwa "intimidation". Wanajaribu kutisha wananchi wasiseme matendo mabaya ya viongozi wa serikali na serikali hususani Rais Samia Suluhu Hassan na CCM yake...
Kwa mfano, yote aliyoyasema huyu binti Sifa Boniventure kwenye wimbo wake ni ya kweli na yanatokea hapa nchini na yanafanywa na viongozi wa serikali hii na kila mtu anajua na wao wenyewe polisi wanajua. Uchochezi ktk mazingira haya unatoka wapi? Kwanini wakosoji na wavunja sheria halisi wanaachwa na kuonea wanaopiga kelele za kukemea uovu?? Ina maana Tanzania tunaongozwa na watoto wa baba wa uovu (shetani) kiasi cha uovu kufunikwa na watawala hawa??
Na uhalisia ni kuwa, serikali hii ya Samia Suluhu Hassan na CCM yake inajichochea yenyewe kwa matendo yake maovu halafu inakamata na kubebesha raia wake wanaousema ushenzi wao. Hii sio sawa na haikubaliki popote mbinguni wala hapa duniani...!
Hii haukubaliki. Ni lazima wamwachie huyu binti mara moja bila masharti yoyote!!