Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Nimesikia kauli za Rais na Makamu wa Rais na zote zinaashiria kuna tatizo kubwa sana kwa mawaziri. Ila bado nashangaa imekuwaje mnawateua inakuwaje mnaendelea nao? Ni kweli huko CCM hakuna watu wengine? Au sio nyie mnaowateua? Ikiwa una mamlaka kamili na unaona Kuna watendaji hawafanyi vizuri si unatengua tu ili kupata watendaji wengine wazuri?
Nakumbuka mama Samia aliwahi kusema anaowatengua ni wale legelege na anawaacha wale ambao wapo vizuri. Ila kwa kauli walizotoa ni wazi bado tatizo ni kubwa sana kuliko kawaida. Makamu wa Rais amezungumzia kauli nzito sana kwa mawaziri, Sasa ni Nani wa kuwawajibisha ikiwa nyie wenyewe mnashangaa na kulalamika?
Kwa muenendo huo wataleta kweli maendeleo kwa nchi na wananchi?