Kauli za wanasiasa juu ya rasimu ya pili ya katiba, "serikali tatu".

Kauli za wanasiasa juu ya rasimu ya pili ya katiba, "serikali tatu".

Joined
Aug 1, 2012
Posts
35
Reaction score
27
KAULI ZA WANASIASA JUU YA RASIMU YA PILI YA KATIBA.
Nimetafakari kidogo kauli za wanasiasa juu ya mapendkezo yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba, Nimeona ni kama vile Rasimu ina ibara moja tuu hususani juu ya Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ambayo inatoa mapendekezo ya Serikali tatu.
Kuna makundi mawili hasimu, moja la kupinga muundo huo la pili la kutetea muundo huo, Sina shaka na hili kundi linalotetea mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya katiba kwani ni matumaini yangu kuwa kile kilichoandikwa ndio mapendekezo ya watanzania walio wengi na ndio maana tume ya mabadiliko ya katiba iliamua kuchukua yale ya walio wengi, hiyo ndio ilikua busara ya wajumbe wa tume ya Warioba.

Kundi hili la pili la kupinga linatoa hoja mbalimbali juu ya kuweka msingi wa pingamizi lao, hususani ni usaliti wa fikra za mwalimu, Pili ni usaliti wa sera za chama Mapinduzi, Tatu sio mapendekezo ya watanzania Nne ni agenda ya kundi la G 55,Tano historia ya Muungano wetu Sita Swala la Ulinzi na Usalama Saba Ni janaga kuwa na serikali tatu, Nane Hakuna watanganyika waliotoa mapendekezo mana hawapo, Tisa Ni Agenda ya Vyama Fulani.
Hoja za hili kundi la pili huenda zikawa na msingi mzuri wa kujadili kwa upana zaidi ikizingatiwa limekosa imani na tume iliyofanya kazi hii ya kukusanya maoni, lakini pili tujadili hoja moja baada ya nyingine, "kwanza ni usaliti wa fikra za mwalimu" Je tulihitaji Rasimu yenye fikra za mwalimu? Kama ndivyo basi twende huko, " Pili ni usaliti wa sera za chama cha mapinduzi" Nayo pia vema iwekwe wazi je tulihitaji rasimu inayoendana na sera za CCM au Sera za Nchi? "Tatu Sio mapendekezo ya watanzania" Je Tume ya Warioba iliwahoji wananchi wa Nchi gani? "Nne ni agenda ya G 55" Je tume iliingia makataba na G55 kwa maslahi ya nani? Au ni mjumbe gani wa Tume ni mmoja wa kundi la G55? "Tano Historia ya Muungano wetu" Je tulihitaji mapendekezo yak u=ihistoria kupata aina ya Muungano "Sita Swala la ulinzi na usalama" Je mambo hayo ya ulinzi na usalama katika rasimu mpya ya utofauti gani na mfumo wa sasa? Au tuu kutaka hoja iwe na sauti kubwa? "Saba Serikali Ttau ni Janga" Ni vema ikawekwa wazi Janga kwa Nani kama ni Janga kwa Chama cha Siasa hivi wananchi tuna maslahi gani kwa Chama kimoja cha Siasa kuondoshwa madarakani? "Nane hakuna watanganyika waliotoa maoni" Je tulihitaji maoni ya watanganyika kupendekeza muundo wa Muungano? Au tulihitaji watanzania watoe mapendekezo ya muundo wa serikali ya muungano? "Tisa Serikali tatu ni agenda ya vyama Fulani" Je ni vibaya vyama kubeba agenda za wananchi na kuzisemea? Na kama ni agenda ya hivyo vyama je ninyi chama chenu agenda yake ni ipi?

Ni vema sasa tukaja na hoja zenye uwingi wa mawazo yenye kujenga na sio kuwa na hoja zenye matamanio binafsi na sio kwa upana wa kitanzania na maendeeleo yake, Lakini pili tujifunze kuwa na adabu katika maamuzi ya wananchi wenye mamlaka makubwa, Mfumo wa chama kushika hatamu sio sasa, muda wa kuishi kwa kudumisha fikra za Mwalimu sio sasa, Muda wa kuzungumza agenda za Chama sio sasa, ni wakati kutambua jamii inahitaji nini nma ndio malengo ya kuundwa kwa tume ya kuchukua maoni kwa wananchi.

Ikumbukwe hiki sio kitu kigeni, Waziri wa wakati huo alisema hatuna haja ya kuwa na katiba mpya, lakini pia yalisemwa hakuna haja ya kujadili Muungano katika mapengdekezo ya awamu ya kwanza kwa tume lakini tume ilihitaji maoni juu ya muungano, utayari wa watawala kubadili aina ya muungano ulikuwa haupo tangu mwanzo wa safari hii waliyolazimishwa kuianza na leo tunataka wafike kama tulivyowalazimisha kuianza halafu tunategemea watafika kwa hiari, ni makosa makubwa sana kama tukiamini hivyo.

Tumeona juhudi za kuaminisha umma juu ya ubovu wa mapendekezo ya tume ambazo zinafanywa na chama cha mapinduzi kwa makusudi kubadili mapendekezo ya umma kuwa sio ya umma na ni ya Warioba na tume yake, leng likiwa ni kukinusuru Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2015, bado naona nia mbaya ya CCM kutothamini hata fursa walioipata kwa njia haramu ya kuwaon goza watanzania na wanahitaji kuirudia tena.
Swala la muundo wa serikali tatu litaligawa bunge maalumu la katiba katika makundi mawili, na ndio mana tume ilivunjwa kwa nguvu kubwa ili CCM ijitathmini wapi ilikosea kama sio makosa ya kumchagua Jaji Warioba kuwa Mwnyekiti wa Tume hiyo, CCM inatumia mbadala wa uteuzi wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, Wajumbe hao kwa hali ilivyo sasa na mikakati ndani ya CCM tayari majina yamefikishwa katika secretariat ya Chama cha Mapinduzi kwa Siri ili kufanya upembuzi na kupendekeza kwa Rais watakao chaguliwa, hii ni kufanya wajumbe watakao teuliwa wengi wao waangaliwa kwa kuzingatia misiamamo yao juu ya muungano na muundo wake.

Hii ni vita ya WANANCHI na CCM juu ya aina ya Muungano je nani atakuwa mshindi ? Jakaya Kikwete aliwahi sema hakuna atakaye kuwa mshindi katika mchakato huu wa katiba, msemo huu hauwezi kuwa sahihi kama upande mmoja unaandaa mkikakati ya ushindi halafu mshindi asipatikane. Wananchi wanahitaji kutumia haki zao za kikatiba kushiriki vema katika mchakato huu hadi kufikia hatua ya upigaji wa kura ya maamuzi ndio wataamua juu ya mambo ambayo wanahisi yanahitaji ufumbuzi kwa maslahi ya watanzania wote.

Naomba kutoa wito kwa watanzania wote kundelea kusimamia msimamo wa mapendekezo yao kwa tume kwani hakuna mapendekezo yaliyoelekezwa nje na tume hivyo hofu isiwepo kwani fursa ya kutoa maamuzi katika hatua ya kura ya maamuzi itakuja na kwa pamoja tutonesha nani mkweli kati ya Tume ya Warioba na Chama Cha Mapinduzi.
 
nitarudi bado natafuna kwanza waraka wako mkubwa na uliosheheni upembuzi mzuri na wa kina ,nawaachia wataalamu wa mambo hayo angulie kwanza kuleta michango yao
 
Walitakiwa wapitishe karatasi nyeupe tuulizwe hivi,
1 Muungano tunautaka au hatuutaki
2 Kama tunautaka Je ni muungano wa aina gani tuutakao?
Ila kwakuwa hatua muhimu ilirukwa ndiyo maana unaona watu wanajitokeza kutetea serikali 2 kwa nguvu zote utadhani wametumwa, Muungano ni wawanachi hata wakitaka muungano wa serikali 1,2,3 4,5 au6 hakuna atakaye wakataza.
 
Back
Top Bottom