''Kausha damu" waliupisha upepo kisha wamerudi tena kwa kishindo

''Kausha damu" waliupisha upepo kisha wamerudi tena kwa kishindo

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 43:
Siku hizi kumekuwa na vibanda vingi sana mitaani almaarufu "Kausha Damu" ambavyo vinakopesha pesa kwa watu wa hali ya chini kwa riba kubwa, mikataba migumu, na masharti ya kusaga meno. Na pindi wakopaji wanapochelewesha marejesho wanaporwa mali zao bila utaratibu mzuri, kama vile viwanja, mashamba, TV, kabati, makosheni, friji, redio, meza, n.k.

Licha ya kuwa mwaka huu (2024) kulipita upepo wa kuwatikisa "Kausha Damu wa mitaani" lakini bado huko mikoani hali imerudi tena kwa kishindo, ni kama Kausha Damu walipisha upepo upite na sasa wamerudi tena. Siku hizi kila mtu akipata hela anafungua kibanda cha kukopesha bila kuwa na leseni kutoka BOT kwa mujibu wa sheria ya mikopo midogo (sheria No.10, 2018 - kifungu cha 16) ambacho kinakataza biashara ya mikopo midogo pasi kuwa na leseni ya Benki kuu.

MAONI: Nipende kutoa maoni yangu kwa BOT na wadau wengine wanaohusika, watoke maofisini waende mtaani kufanya operesheni maalum ya kuwasaka "Kausha Damu" ambao wanatoa huduma ya mikopo bila kuwa na leseni ya Benki kuu. BOT mkifanya hivyo itasaidia kuwapunguzia adha wananchi wa hali ya chini.

Soma Pia: Kausha damu ni changamoto kwa waalimu

Right Marker
Dar es salaam
 
Back
Top Bottom