Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohammed Kawaida amemjibu aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akisema kazi ya usafirishaji abiria kwa kutumia bodaboda si laana, bali ni kazi iliyoajiri vijana wengi.
Machi 2023 baada ya kurejea nchini akitokea Canada, Lema alisema bodaboda sio ajira, ni umaskini uliopitiliza na hatarishi. Aliwataka vijana wa bodaboda kukemea ajira hiyo ya laana huku akisisitiza kwamba "hamuwezi kufanya ajira ya kukimbiza upepo kwa Sh7, 000 kwa siku."
Akizungumza na Umoja wa Waendesha Bodaboda Arusha leo Desemba 27, 2024, Kawaida amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakidai kazi hiyo ni ya laana, lakini si kweli, ba.li kazi hiyo imeajiri vijana wengi nchini Tanzania na imesaidia kupunguza tatizo la ajira.
Akihutubia vijana hao wa bodaboda, Kawaida ameitaja sekta hiyo kuwa muhimu kiuchumi, akiwataka kujisimamia kikamilifu na kujiepusha kutumika kisiasa katika kuchafua viongozi.
Mwenyekiti huyo, amewakumbusha vijana hao kufuata sheria za usalama barabarani, taratibu walizojiwekea na kujiepusha na ulevi wakati wa kazi.
Soma, Pia: Rais Samia atoa milioni 10 kwa Boda boda Arusha