Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
KOMREDI MOHAMMED KAWAIDA ATAKA TIJA KILIMO BBT
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa Ndugu Mohamed Ali Kawaida amewataka vijana nchini kutokidharau Kilimo na badala yake wakikumbatie na kuiona kama kazi itakayowainua kimaendeleo.
Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (Building Better Tomorrow-BBT) eneo la Bihawana Dodoma ambapo vijana 73 wanafundishwa stadi mbalimbali za kilimo, Kawaida amesema, vijana wakikiona kilimo ni biashara watajikwamua kiuchumi.
Katika kutembelea mradi huo unaotekelezwa katika maeneo 13 nchini huku ukiwakusanya pamoja vijana 812 kwa kuanzia. Mwenyekiti Kawaida aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhe. Gerald Mweri.