Kawaida Awakosoa Wasomi Mradi wa BBT
MOHAMMED KAWAIDA AWAKOSOA WASOMI MRADI WA BBT
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Mohamed Kawaida ameitaka jamii kuondokana na dhana kwamba mradi wa Jenga Kesho Iliyobora BBT kuwa umeletwa kwa ajili ya wasomi pekee na badala yake unakusanya makundi yote ya vijana.
Akizungumza katika kitalu Atamizi cha BBT Bihawana Mkoani Dodoma alipotembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana 73 waliopo mafunzoni, Kawaida amesema mradi huo umekusanya wenye shahada, wahitimu wa darasa la saba na hata watu wenye mahitaji maalum yaani wenye ulemavu wa kutoona.
Kwa sasa zaidi ya vijana 812 wako katika mafunzo haya ya kilimo katika vituo mbalimbali nchini, kijana yeyote wa Kitanzania ana sifa ya kujiunga na mradi huu pale fursa nyingine zitakapotangazwa.
-
Ft607fdXwAEri16.jpg
189.7 KB
· Views: 17