Zambotti
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 1,973
- 3,643
Juzi katika pitapita zangu sokoni Kariakoo nimeshuhudia matukio yakushangaza yanayofanywa na hawa jamaa ambao tshirt zao mgongoni zimeandikwa KAWASCO.
Kwanza wanatembea kwenye kikundi cha watu saba mpaka kumi.
Shughuli yao kuu ni kuondoa wafanyabiashara ambao hawajajipanga kwenye maeneo rasmi hususani wasiokuwa na vimeza.
Wanakamata wale wanaopanga chini na wanaotembeza mikononi.
Kinachohatarisha maisha yao ni aina ya ukamataji wao na lile fujo linalotokea baada ya ukamataji.
Hii inaleta picha kwamba hawa ndio mgambo mpya wa jiji kwa eneo la soko la kariakoo, lakini bila shaka ni watu wa kampuni binafsi ambao wanapambana na machinga watembeza bidhaa mikononi.
Kama wataendelea na mwendo huu basi tukae tayari kupokea taarifa mbaya kuwahusu hawa jamaa kama ile ishu ya afisa wa LATRA kutolewa panga akiwa kwenye majukumu yake.
Nawasilisha.