KAWASCO mgambo wa Kariakoo wako hatarini

Zambotti

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
1,973
Reaction score
3,643
Juzi katika pitapita zangu sokoni Kariakoo nimeshuhudia matukio yakushangaza yanayofanywa na hawa jamaa ambao tshirt zao mgongoni zimeandikwa KAWASCO.

Kwanza wanatembea kwenye kikundi cha watu saba mpaka kumi.

Shughuli yao kuu ni kuondoa wafanyabiashara ambao hawajajipanga kwenye maeneo rasmi hususani wasiokuwa na vimeza.

Wanakamata wale wanaopanga chini na wanaotembeza mikononi.

Kinachohatarisha maisha yao ni aina ya ukamataji wao na lile fujo linalotokea baada ya ukamataji.

Hii inaleta picha kwamba hawa ndio mgambo mpya wa jiji kwa eneo la soko la kariakoo, lakini bila shaka ni watu wa kampuni binafsi ambao wanapambana na machinga watembeza bidhaa mikononi.

Kama wataendelea na mwendo huu basi tukae tayari kupokea taarifa mbaya kuwahusu hawa jamaa kama ile ishu ya afisa wa LATRA kutolewa panga akiwa kwenye majukumu yake.

Nawasilisha.
 
umenikumbusha kuna mgambo mmoja hapo kariakoo alikuwa anawaletea fujo wamachinga kumbe mtaani anapokaa ndio wamachinga wanapoishi sikosei kama
mbagara au gongo la mboto.kilicho mtokea walimpiga visu ila alipona
 
So sad
 
Ukileta ugomvi kwenye sehemu ya wenzio kula au kutafutia mia mbili mia tatu ujiandae kisaikolojia, watu wana weza waka kuvizia waka kutoa hata marinda ohoooo..! [emoji16]
 
Lianzishe afu uone nani ataumia
 
Hata Jana niliona wanapakia vitu vya watu nkasema Dah Yan watanzania waliokuwa wanafanya biashara kwa uhuru wamekuwa watu wa kukimbia kimbia kwenye nchi yao wenyewe asee nimesikitishwa sana
 
umenikumbusha kuna mgambo mmoja hapo kariakoo alikuwa anawaletea fujo wamachinga kumbe mtaani anapokaa ndio wamachinga wanapoishi sikosei kama
mbagara au gongo la mboto.kilicho mtokea walimpiga visu ila alipona
Usifanye mchezo na sehemu watu wanapotafuta riziki zao kulisha familia ni hatari sana
 
Ila usisahau kusema kama wewe machinga wa mtaa gani hapo 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…