Uchaguzi 2020 Kawe kunani? Why is a hot cake? Wamejitokeza wagombea 176! What is so special ? Kuchinja watu 175 kubaki 1, is not a joke!.Je, atakuwa nani?

Wewe Pascal Mayalla ni chakubanga chakubanga huna hoja kafanye mambo yenu ya gizani ukalale. Huaminiki hata na kuku.
 
Zamani ulikua unajinasibu kuwa wewe sio mwanachama wala mkereketwa wa chama chochote cha siasa yaani upo neutral ila sikuhz
Zamani ulikua unajinasibu kuwa wewe sio mwanachama wala mkereketwa wa chama chochote cha siasa yaani upo neutral ila sikuhz unaonesha kabisa upande wako halisi.....hahaaaaaaa
 
Siyo atakayepatikana atakuwa best of the best CCM huwa haifanyi kazi namna huyo mkuu Paschal. Anaweza akawepo mtu bora kuliko wote na akashinda kura lakini akakatwa akawekwa boya wanaomtaka wao. CCM haina demokrasia kwa swala la kukata watu. Ndiyo maana Iringa mtu ambaye ambaye angeshinda walimkata wakaweka boya akapigwa na Msigwa wakajuta.
 
Ni hatari kweli hadi Paul Mashauri naye yumo kwenye kinyang'anyiro ,siri ya kujitokeza wengi ni kwamba wamemkubali magufuli.
Huu ndio upuuzi huwa sitaki kabisa kusikia. Eti mtu anagombea ubunge kwa sababu ya kumkubali Rais? Uongo wa kijinga kabisa!
Rais ni kiongozi wa mhimili mwingine uitwao serikali, unagombea ubunge ambao upo ndani ya muhimili ambao kazi yake ni kuikemea serikali na kuisimamia itimize wajibu wake vizuri. Mahusiano ya kufanya mtu ahamasike kugombea yako wapi?
Au ni kutokujua wajibu wa mbunge ni nini? Nakumbuka niliwahi msikia Mbunge Sugu akisema hata Rais akitokea Chadema, tutamtwanga bungeni na pia katika vikao vya chama atatwangwa ili nchi ifuate sheria, katiba na kanuni zake. Huo ndio ubunge.
Sasa hizo takataka za eti "nagombea kuunga mkono juhudi" kama sio umbumbumbu ni nini?
 
Pasco tumekee hapa list ndo tutajua atakuwa nani.
 
Masahihisho kidogo,

Wananchi wanaweza kumkataa mgombea mmoja tuu kati ya hao 176.

Maana hatapita mtia nia no1 mpka 176, mbele ya wananchi, huku wakiulizwa.

"Ndio huyu, siyo". 'Na huyu je"

Kukataliwa kwa mgombea mmoja wa CCM(atakae pitishwa na CCM) haimaanishi, wananchi wamewakataa wote 176.

Hivyo basi CCM wahakikishe wanapitisha "the best of 176".
 

Kungekuwa na uchaguzi hapo sawa, ila sio kwa huu uchaguzi ambao tayari Magufuli kashaagiza nani atangazwe mshindi.
 

Ugumu utoke wapi Paskali hapo, atakayepatikana ni yule atakayekuwa amepewa ajenda ya kumuongezea Magufuli muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Huo wingi ni kuhadaa umma tu kuwa ccm kuna demokrasia, jambo ambalo si kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…